Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakurugenzi kutosheherekea sikukuu
ya Christmas mpaka watakapopata ufumbuzi wa ujenzi wa madarasa 99
yanayohitajika kwaajili ya kutumiwa na wanafunzi 4930 waliofaulu kuingia kidato
cha kwanza mwaka 2019.
Amesema
kuwa ufaulu mwaka huu 2018 umekuwa kwa asilimia 73 ukilinganisha na mwaka 2016
ambapo ulikuwa ni wa asilimia 68 na hivyo wanafunzi 4930 kukosa kuingia
madarasani kutokana na changamoto ya upungufu wa madarasa.
Ameongeza
kuwa serikali ya Mkoa imejipanga vilivyo kuhakikisha hakuna hata mwanafunzi
mmoja anakosa nafasi ya kusoma hali ambayo itawafanya wanafunzi wote waliokosa
nafasi kupatiwa fursa ya kuendelea na masomo yao kwa mwaka 2019 na kuwaomba
wanachi kwa kushirikiana na halmashauri kuhakikisha vyumba hivyo vinapatikana
hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa pili.
“Hawa
wanafunzi tusiwakatishe tamaa ya kukosa nafasi ya kwenda kidato cha kwanza,
hakuna mwanafunzi hata mmoja ataacha kwenda kidato cha kwanza, wakuu wa wilaya
wote wasimamie zoezi hili na hakuna likizo na wale wakurugenzi wote hakuna
kwenda likizo mpaka vyumba vya madarasa vyote view vimekamilika,” Alisema.
Ametoa
maagizo hayo wakati akitoa salamu zake za Christmas kwa wananchi wa mkoa wa
Rukwa na kuwatakia wananchi wote kusherehekea sikukuu hiyo pamoja na
kuukaribisha mwaka mpya kwa amani na utulivu kwani walianza vizuri na wamalize
vizuri na kuwaomba kuendeleza mshikamano na ushirikiano kwa miaka inayofuata.
Kati ya
hayo madara 99, halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inatakiwa kujenga
madarasa 41 yatakayotumiwa na wanafunzi 2,042, huku Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga ikihitaji madara 27 ili kutumiwa na wanafunzi 1,365 na halmashauri
ya Wilaya ya Nkasi ikihitajika kujenga madarasa 19 kwaajili ya wanafunzi 925 na
halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikitakiwa kujenga madarasa 12 kwaajili ya
wananfunzi 598.
0 comments:
Post a Comment