Waziri wa Madini Angellah Kairuki sambamba na Naibu Waziri Doto Biteko katikati mbele) wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Umahiri cha Musoma
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia ubora wa nondo zinazotumika katika ujenzi wa Kituo cha Umahiri.
Ø Asema baada ya Lwamgasa
kituo kingine cha mfano kujengwa
Imeelezwa
kuwa, vituo vya Umahiri vinavyojegwa maeneo mbalimbali nchini vinatarajiwa kuwa
kichocheo cha shughuli za uongezaji thamani madini nchini kwa kuwa, vinatarajia
kutoa mafunzo ya uchimbaji bora wa madini ikiwemo uongezaji thamani madini,
ukataji na ung’arishaji madini.
Hayo
yamebainishwa Novemba 20 na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati alipofanya
ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Umahiri cha Musoma
kinachojengwa na Mkandarasi kampuni ya SUMAJKT na kusimamiwa na kampuni ya Sky
Architects.
Katika
ziara hiyo, Waziri Kairuki ameambatana na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkurugenzi wa
Sera na Mipango Augustine Ollal, Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa
Rasilimali Madini, Andrew Eriyo pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Mara na uongozi wa
Mkoa wa Mara.
Waziri
Kairuki ameeleza kwamba, serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa shughuli za
uongezaji thamani madini zinafanyika nchini badala ya kusafirisha madini yakiwa
ghafi na kuongeza kuwa, uwepo wa vituo
husika utaongeza shughuli hizo kufanyika
nchini kwa kuwa vitatoa elimu ambayo
itawezesha wachimbaji kufanya uchimbaji wenye tija.
Pia,
amesema serikali itaendelea kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini
kufanyika nchini ikiwemo kuhakikisha kwamba inajenga maeneo mengi zaidi ya vituo hivyo.
Vilevile,
amezungumzia kituo cha mfano cha Lwamgasa kinachojengwa mkoani Geita, na
kueleza kuwa, serikali inaangalia uwezekano wa kuwa na kituo kama hicho katika
maeneo mengine na kuongeza, “tunaangalia sehemu nyingine baada ya kuwa na kituo
cha mfano cha Lwamgasa huenda tukajenga kituo kama hicho hapa Musoma”.
Kituo
cha Lwamgasa ni moja ya vituo ambavyo vinalenga katika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya
dhahabu kuhusu uchimbaji wenye tija ikiwemo uchenjuaji bora pasipo kutumikia
kemikali.
Kwa
mujibu wa taarifa ya wizara ya tarehe 29 Oktoba, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini, wizara ilieleza kuwa kazi ya ujenzi wa mgodi wa Lwamgasa na usimikaji
mitambo ya uchenjuaji katika kituo hicho
imekamilika kwa asilimia 80.
Akiwa
kituoni hapo, Waziri Kairuki ameendelea kusisitiza kuhusu kuzingatia muda wa
kukamilisha ujenzi huo ikiwemo kuzingatia ubora na viwango vya ujenzi
vinavyotakiwa.
Pia,
ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa ushirikiano inaoonesha katika kufuatilia ujenzi
huo na kuutaka kuendelea kushirikiana na wizara ili kuhakikisha kwamba azma ya
kituo hicho inafikiwa.
Kwa
upande wake, Afisa Madini Mkoa wa Mara, Mgaya Nyaisara amesema kuwa, kituo kitatoa mafunzo ya namna
ya uandaa sampuli za madini, namna ya kusafisha madini pia kutakuwa na mashine
za kupima madini ya aina mbalimbali.
Naye
w Mkandarasi SUMAJKT, katika taarifa iliyosomwa na Meja Onesmo Njau, amesema
kuwa, kampuni hiyo itahakikisha inakamilisha ujenzi wa kituo hicho katika muda
uliopangwa kimkataba na kueleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho unaogharimu
shilingi bilioni 1.2 ikijumuisha jengo la ofisi ya madini na kituo cha umahiri
umefikia asilimia 35.
Vituo
vya umahiri vinajengwa kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini
(SMMRP) kwa Benki wa Dunia
0 comments:
Post a Comment