Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu Hassan akipata maelezo ya umuhimu wa zabibu ya Dodoma katika uzalishaji mvinyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alkovintages Bw. Archard Kato (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa tamasha la mvinyo Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni kwa mchango wa nchi yake katika kusaidia kilimo cha zabibu wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito maalum kwa Wakulima, Wajasiriamali na wadau wa sekta zingine kuhakikisha kuwa bidhaa zinafikia ubora wa hali ya juu kuanzia shambani zinakozalishwa, zinakosindikwa na kufifadhiwa hadi kumfikia mlaji.
Makamu wa Rais ametoa wito huo leo wakati hafla ya Uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo lililofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma.
“Niwaase Watanzania kupenda vya kwetu maana waswahili husema thamini chako mpaka cha mwenzako usikione kama kitu” alisema Makamu wa Rais
Makamu wa Rais amewataka wakazi wa Dodoma kutumia maonyesho hayo kama fursa ya kujifunza teknolojia mbalimbali zinazoweza ongezeko la tija, teknolojia za usindikaji na usambazaji wa bidhaa zinazozalishwa kwa zabibu.
Mkoa wa Dodoma unazalisha wastani wa tani 2.25 ikilinganishwa na tani 8 kwa wakulima wanaozingatia kanuni bora za kilimo.
Serikali inaendelea kusambaza umeme vijijini, kuboresha miundombinu ya barabara, maji na kuhakikisha wakulima wanapata mikopo yenye masharti nafuu kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwani kufanya hivi kutaharakisha pia jitihada za wakulima kuwa na viwanda vya usindikaji ambavyo vitapandisha thamani zao lao.
Aidha, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali imeongeza zao la Zabibu katika orodha ya mazao ya kimkakati lengo likiwa kuongeza uzalishaji na tija kwa mkulima.
0 comments:
Post a Comment