Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maandalizi
ya ujenzi wa madaraja ya kupitisha treni juu
wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya
Kisasa ya SGR Oktoba 3, 2018. Kambi hiyo ipo eneo la Shaurimoyo jijini
Dar es salaam. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi, Isack Kamwelwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya utengenezaji mataluma ya reli ya SGR wakati alipotembelea Kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utandikaji wa Reli ya SGR katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Ni baada ya kuhakikishiwa kipande Dar-Morogoro kitakamilika Aprili 2019
badala ya Julai
WAZIRI Mkuu
Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa
reli ya kisasa (SGR) inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi.
Amesema kipande
cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 ambacho
kilitakiwa kukamilika Julai 2019, wataalamu wamesema watakamilisha Aprili 2019.
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa
reli ya kisasa kuanzia eneo la Shaurimoyo Dar esSalaam hadi
Soga, Pwani.
“Nimeridhishwa
na viwango na maendeleo ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa
Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii.”
Waziri Mkuu
amesema Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka
kuona SGR inakamilika na kuanza kutumika nchini yanatimia.
Kuhusu suala la
ajira, Waziri Mkuu amesema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa
katika mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.
“Watanzania
mnaofanya kazi katika mradi huu hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa
bidii, uaminifu na muwe mabalozi wazuri ili wengine waweze wapate ajira.”
Awali,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa
alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli kutoka Dar es Salaam
hadi Makutupora unagharimu sh. trilioni 7.1.
Alisema mradi
wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza
umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam
hadi Morogoro chenye urefu km 300 na kitagharimu sh. trilioni 2.7.
“Kipande
kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa km. 422 ambacho
kitagharimu sh. trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora km. 376.5, Tabora hadi
Isaka km 162.5 na Isaka hadi Mwanza km. 311.25.”
Mkurugenzi huyo
alisema kukamilika kwa reli hiyo ya kisasa kutachochea mipango ya Serikali
katika kutekeleza sera ya viwanda na kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025.
Pia reli hiyo
itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati
hususan kwa nchi zisizopakana na bahari kwani watasafirisha mizigo yao kwa
haraka na uhakika.
Akizungumzia
mradi huo kwa ujumla, Kadogosa alisema maendeleo ya mradi huo ni asilimia 32
kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro na asilimia 3. 31 kwa kipande cha
Morogoro-Makutupora.
0 comments:
Post a Comment