Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko akihutubia wananchi wa kijiji cha Ngula na
wachimbaji wadogo wadogo wa mgodi wa Nyati Resources Ltd (hawapo pichani)
katika mkoa wa Geita tarehe 2 Novemba, 2018
Mkazi
wa kijiji cha Ngula, Mindi Masasi (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa
Madini, Dotto Biteko (hayupo pichani). Katikati ni Mtoto wa Mindi Masasi, Makanika Chalo pamoja na Mwenyekiti wa kata ya
Bujula (jina halikupatikana)
Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngula mara
baada ya kukagua Mgodi wa Nyati Resources Ltd uliopo katika kijiji cha Ngula
kata ya Bujula mkoani Geita.
Na Rhoda James - Geita
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza mgodi wa Nyati Resources ltd uliopo
katika kijiji cha Ngula kata ya Bujula mkoani Geita kutolipa gawio Serikali ya
kijiji cha Ngula kuanzia tarehe 2 Novemba, 2018 ili kutoa nafasi ya uchunguzi
kujua ni nani mmiliki halisi wa eneo hilo la mgodi.
Ametoa
agizo hilo wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 2 hadi 3
Novemba, 2018 iliyolenga kukagua machimbo
ya madini katika Mkoa wa Geita.
Pamoja
na ukaguzi huo, Biteko ameeleza kuwa, ametembelea machimbo hayo ili kutatua
mgogoro wa ardhi uliopo baina ya Kijiji cha Ngula na mkazi wa kijiji hicho
Mindi Masasi.
Akizungumza
katika kikao hicho, Biteko ameutaka Mgodi huo wa Nyati Resources ltd kutolipa
gawio kwa kijiji hicho kwa kuwa kuna malalamiko kutoka kwa mkazi wa kijiji
hicho ambaye ni Mindi Masasi.
Biteko
ameeleza kuwa mgodi huo umeanza uzalishaji tangu Desemba, 2017 na umekuwa ukimlipa
Mindi Masasi gawio kwa zaidi ya mwaka kwa kuwa wakati wanaanza uzalishaji wa
dhahabu wamemkuta katika ardhi hiyo ambayo amekuwa akiishi tangu mwaka 1954
lakini sasa kijiji kinadai kuwa ardhi hiyo ni mali yao na wao ndio wenye haki
ya kulipwa gawio hiyo.
Pamoja
na maswali mengi yanayojitokeza, Biteko amesema ni vyema tuachie mamlaka husika
kufanya uchunguzi kuhusiana na suala hili “Zaidi ya mwaka Masasi amekuwa
akilipwa gawio na mgodi huu, je serikali ya kijiji cha Ngula ilikuwa wapi,
mbona serikali ya kijiji haizungumzii eneo lingine isipokuwa eneo la mgodi,”
aliuliza Biteko.
Wakati
huo huo Biteko ameutaka Mgodi wa Nyati Resources ltd kutoa maelezo ni kwa nini
tangu mwaka 2017 Desemba walipoanza uzalishaji wa dhahabu wamelipa Mrabaha wa
kiasi cha Shilingi 200,000/- tu wakati mapato yao ni zaidi ya milioni 50.
“Huo
ni ukiukwaji wa ulipaji wa kodi za Serikali, haiwezekani tangu mwaka jana hadi
leo mmefanikiwa kulipa Mrabaha wa laki mbili tu,” alisema Biteko.
Aliongeza
kuwa lazima wazawa kuonesha mfano mzuri wa kulipa kodi ili hata wawekezaji
kutoka nje ya nchi wakija waone umuhimu wa kulipa kodi.
Kwa
upande wake Meneja wa Mgodi wa Nyati Resource ltd, Christopher Nilla amekiri
kuwa kweli kumekuwepo na mapungufu katika ulipaji wa kodi za Serikali lakini na
kuahidi kubadilika na kulipa sawasawa na sheria ya madini na kubainisha kuwa wanamiliki mgodi mwingine ambapo zaidi ya Tsh
milioni kumi zimelipwa serikalini.
Captions
Pic
1
Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko akihutubia wananchi wa kijiji cha Ngula na
wachimbaji wadogo wadogo wa mgodi wa Nyati Resources Ltd (hawapo pichani)
katika mkoa wa Geita tarehe 2 Novemba, 2018
Pic
2
Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngula mara
baada ya kukagua Mgodi wa Nyati Resources Ltd uliopo katika kijiji cha Ngula
kata ya Bujula mkoani Geita.
Pic
3
Mkazi
wa kijiji cha Ngula, Mindi Masasi (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa
Madini, Dotto Biteko (hayupo pichani). Katikati ni Mtoto wa Mindi Masasi, Makanika Chalo pamoja na Mwenyekiti wa kata ya
Bujula (jina halikupatikana)
0 comments:
Post a Comment