METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 5, 2022

ONASTORIES YAWEZESHA VIJANA KWENYE SHINDANO LA DUKUZI ZA KIBUNIFU ZA TEKNOLOJIA


Na Andrew Chale, Dar es Salaam

Kampuni ya ONASTORIE imewezesha Wabunifu wa Kitanzania wakiwemo Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali Nchini kushiriki kwa mara ya kwanza shindano la dukuzi za Kibunifu kwenye upande wa Teknolojia ya Uhalisia ongezi.

OnaStories wameendesha mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika ukumbi wa Dlab Kijitonyama Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wadau kampuni ya META (zamani Facebook),IMISIED,Dlab na Blackrhino ambapo mwisho washindi walizawadiwa zawadi ikiwemo fedha za kusaidia bunifu zao.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo, Mshirika mwenza wa kampuni hiyo,Bi. Tulanana Bohela alisema kuwa, mafunzo hayo ni kwa mara Kwanza yanafanyika nchini yakisimamiwa na OnaStories huku yakifanyika pia nchi zingine 16, 

ambapo washindi wa jumla watakutana pamoja kwa Bara la Afrika katika mafunzo makubwa zaidi hapo baadae.

"Tanzania ikiwa ni miongoni mwa Nchi 16 Barani Afrika ikiwa ni zaidi ya washiriki 1,000, OnaStories ikiwa ndio muendeshaji mkazi wa Udukuzi huo hapa nchini, ikiweza kupata makundi kumi yaliyoshiriki kikamilifu ndani ya siku hizo tatu za kutafuta (kudukua) wazo tatuzi na lenye manufaa katika jamii ya Kitanzania". Alisema Tulanana Bohela 


Na kumalizia kuwa, mawazo hayo yalijikita kwenye sekta ya elimu, afya, utalii, Biashara na ubunifu ambapo Udukuzi huo ukiwa ni muendelezo wa hatua ya awali ya Pre-Hackathon ambapo washiriki walikutanishwa na wataalamu kutoka pande zote za Afrika na kufundishwa mbinu mbalimbali na njia bora ya kutumia na kutengeneza wazo kupitia teknolojia za Uhalisia ongezi." Alisema Tulanana Bohela.

Washindi katika shindano hilo, kundi la kwanza walizawadiwa dola 1,500 Usd na kupata nafasi kwenye mashindano makubwa zaidi ya Bootcamp yanayoanza January hadi mwezi April, ambapo itakaribisha nchi 16 za Afrika.

Aidha, washindi wengine wakiwemo Washindi wa pili walizawadiwa dola 800 huku mshindi wa tatu dola 700.

Aidha, washiriki washindi wa Kwanza kutoka hapa nchini watashiriki Mashindano ya Afrika yanayofahamika kama Bootcamp ambapo mshindi wa kwanza wa nchi zote 16 zitakazoshiriki na huko watapita miezi mitatu ya mafunzo, maboresho ya mawazo yao na ushindani.

"Hii Bootcamp itakua Januari hadi April, Mshindi wa kwanza atapatiwa dola 10,000, wa pili dola 8,000 na watatu atapatiwa dola 7,000

Mwisho
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com