Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa
Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa
Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi
Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha,
Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimuonyesha viungo vya chai kutoka Zanzibar Balozi wa Japan nchini Mhe.
Shinichi Goto (kushoto) wakati wa kumkabidhi kama zawadi, Mheshimiwa Balozi wa
Japan alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Hamdi
Abuali, Balozi wa Palestina; Mhe. Shinichi Goto, Mhe. Balozi wa Japan na Bwana
Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.
Makamu wa Rais alianza kuonana na Mhe. Hamdi
Abuali, Balozi wa Palestina , hapa nchini aliyekuja kwa lengo la
kujitambulisha.
“Katika mazungumzo yetu alinielezea kuhusu hali ya
kisiasa ya Palestina na uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwishoni mwa mwaka
huu” alisema Makamu wa Rais.
Balozi huyo pia alimueleza Makamu wa
Rais jinsi anavyo furahishwa na utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwenye kujenga Tanzania mpya
yenye kuendeshwa na uchumi wa viwanda.
Makamu wa Rais alipata nafasi ya kufanya mazungumzo
na Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye alikuja kwa lengo la kujitambulisha.
Balozi huyo aliwasilisha salamu za Mhe. Shinzo Abe,
Waziri Mkuu wa Japan na kueleza utayari wa Japan kuendelea kutusaidia katika
kukuza uchumi.
Makamu wa Rais ameipongeza Japan kwa kuchaguliwa
kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kibiashara ya ‘World Expo’ kwa mwaka 2025.
Pia Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kumshukuru
Balozi wa Japan kwa mradi wao unaolenga kuboresha maisha ya watu wa hali ya
chini kwenye sekta ya Elimu na Afya.
Vilevile Makamu wa Rais alimueleza Balozi huyo kuwa
ili ushirikiano wetu uzidi kukua basi ni vyema kuhakikisha kuwa tunaendelea
kubadilishana uzoefu ikiwemo kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wa pande zote
mbili wanatembeleana na kunufaika na fursa zilizopo baina yetu.
Mwisho, Makamu wa Rais alikutana na kuzungumza Bwana
Abdulmajid Mussa Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB aliyefika
ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.
Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi huyo alimueleza
Makamu wa Rais shughuli mbalimbali za kibenki wanazotoa kwa Jamii na Serikali
wakiwa na lengo la kuhakikisha huduma hizi hazitoki nje ya lengo la uanzishwaji
wa Benki hii ambalo ni kuwezesha vikundi mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment