Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka Jiwe la Msingi la Soko Kuu la
Kalangalala mjini Geita, Novemba 28, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Geita, Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Soko Kuu la
Kahangalala mjini Geita wakati alipoweka jiwe la msingi la Soko hilo, Novemba
28, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia
wananchi wa Mji wa Geita baada ya kuweka jiwe la Msingi la Solo Kuu la
Kalangalala, Novemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Azitaka halmashauri zingine nchini ziige mfano wa Mji wa Geita
WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwaameweka jiwe la msingi mradi ujenzi wa soko kuu
la Kalangalala katika Mji wa Geita na kuzitaka halmashauri zingine
nchini kuiga.
Pia, amesema wajasiriamali
waliokuwa wakifanya shughuli zao katika eneo hilo kabla ya ujenzi
watakuwa wa kwanza kupewa maeneo ya kufanyia biashara.
Waziri Mkuu ameyasema hayo
leo (Jumatano, Novemba 28, 2018) baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi
kwenye mradi wa soko la Mji wa Geita.
Amesema ni vema halmashauri
zote zikaiga mfano wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kujenga masoko ya kisasa
ili wajasiriamali wapate maeneo ya kufanyia kazi zao.
“Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwaondolea wananchi kwa
kuboresha na kuimarisha huduma za jamii.”
Hivyo, Waziri Mkuu
amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel kwa kuwa mbunifu na
msimamiaji mzuri wa miradi ya maendeleo.
Waziri Mkuu amesema
Serikali inahitaji viongozi wa aina yake, ambao si wabadhilifu bali wanajali
thamani na maslahi ya wananchi katika maeneo yao ya kazi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita,
Mhandisi Gabriel ameahidi kulinda heshima ya wananchi wa mkoa huo
kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Amesema atasimamia
kikamilifu ujenzi wa miradi ya maendeleo, ukiwemo ujenzi wa soko la kisasa
ambalo litakapokamilika wajasiriamali watafanyakazi muda wote hadi usiku.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa
Mji wa Geita, Adolf Ritte amesema ujenzi wa mradi huo umegawanyika katika awamu
mbili, ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa soko lenye majengo makubwa
mawili yenye thamani ya sh. bilioni 1.9.
Amesema kukamilika kwa
mradi huo kutawanufaisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wananchi
watakaokuwa wanakwenda kununua bidhaa mbalimbali kwenye soko hilo.
“Pia Halmashauri ya Mji
nayo itanufaika kwa kuongezeka kwa mapato yake ya ndani. Ajira zitakazozalishwa
sokoni hapo ni takribani 200. Faida nyingine ya mradi huu ni kumaliza mgogoro
wa maeneo ya kufanyia biashara katika mji wetu.”
Mapema leo Waziri Mkuu
alikagua mradi wa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Mji Geita kwenye eneo la
Magogo na kisha alikwenda katika eneo la Bombambili kwa ajili ya kukagua na
kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi za CCM mkoa wa Geita.
0 comments:
Post a Comment