Naibu Waziri wa Madini, Mwl. Doto Mashaka Biteko amefika katika
machimbo (mgodi) ya kokoto Lugoba, Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na
kuridhishwa na utendaji kazi katika machimbo hayo.
Mwl. Biteko ametoa pongezi kwa kampuni ya Yaate Investment kwa
kushirikiana na kampuni ya Yapi Merkezi kwa uwekezaji mzuri unaozingatia sheria
ya madini.
Akiwa katika machimbo hayo, ametoa muda usiozidi siku tano hadi
jumatatu wiki ijayo kwa Bw. Akram Aziz ambaye ametelekeza mitambo/ vifaa yake
ya uchimbaji kokoto katika eneo hilo vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi
yake kwani ni kosa kisheria kutelekeza mitambo hiyo kwenye eneo la leseni ya
uchimbaji lisilo lake.
Ifahamike kwamba malighafi za ujenzi wa reli ya kisasa (Standard
Gauge Railway) zinatoka katika mgodi huo.
Katika hatua nyingine, Mwl. Biteko ametoa msimamo wa serikali wa
kuendelea kuufunga mgodi wa kokoto unaomilikiwa na kampuni ya Lugoba Tan-Turk
Stone Quarry hadi utakawalipa fidia wakazi wanaozunguka mgodi huo ili wapishe
shughuli kuendelea.
Uongozi wa mgodi huo kupitia kwa Mkurugenzi wake, Raci Omary
umeomba kupewa muda hadi mwezi Disemba mwaka huu ili kutoa fidia kwa wakazi
hao.
Sehemu
ya mchanga na kokoto katika mgodi wa kokoto Yaate Investment
Sehemu
ya mchanga na kokoto katika mgodi wa kokoto Yaate Investment
Naibu Waziri wa Madini, Mwl. Doto Biteko akikagua
mgodi wa Lugoba Tan-Turk Stone Quarry ambao umefungiwa.
Naibu Waziri wa Madini, Mwl. Doto Biteko akikagua eneo la upasuaji kokoto katika mgodi wa Lugoba Tan-Turk Stone Quarry
Sehemu
ya mitambo iliyotekelezwa katika eneo la mgodi wa upasuaji kokoto wa Yaate
Investment
0 comments:
Post a Comment