Na Munir Shemweta, WANMM Serengeti
Katika kile kinachoonekana kútekeleza kauli mbiu ya
serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amekagua majalada ya ardhi katika
halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara na kuwapigia simu wananchi
ambao majalada yao yana muda mrefu bila ya kupatiwa hati za ardhi.
Akiwa katika oisi ya kutunzia majalada katika
halmashauri ya Serengeti Mabula alikagua jalada moja hadi jingine na
kubaini badhi ya majalada yakiwa na muda mrefu huku wananchi wakiwa
hawajapatiwa hati ambapo baadhi yake ni za tangu mwaka 2017 na kumhoji
afisa ardhi mteule suala la kuchelewa kuwapatia hati za ardhi pamoja na
wahusika kujaza fomu za maombi.
Mabula alielezwa kuwa baadhi ya wananchi wameshindwa
kupatiwa hati kwa wakati kutokana na kushindwa kukamilisha baadhi ya taratibu
pamoja na jitihada mbalimbali zilizofanywa na maafisa ardhi wa halmashauri
kuwakumbusha jambo lillilomshtua Naibu Waziri kwa kuwa wananchi wengi wamekuwa
na shauku kubwa ya kupatiwa hati.
Katika kujiridhisha na maelezo ya afisa ardhi mteule
wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Mhe. Mabula aliamua kumpigia
mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Stanslaus na kumuuliza kwa nini
hajapatiwa hati katika kiwanja Na 619 kitalu B Chamoto wakati aliwasilisha
maombi ya kupatiwa hati.
Mwananchi huyo alipopokea simu na kuelezwa kuwa
aliyekuwa akiongea naye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
na alikuwa akihoji maombi yake ya hati ya ardhi aliyoyawasilisha ofisi za
halmshauri ya wilaya ya Serengeti, alishangaa kwa kuwa muda
aliopigiwa simu majira ya saa kumi na mbili jioni haukuwa muda wa kazi.
Mwanachi huyo mkazi wa Mugumu wilaya ya Serengeti
alimueleza Mabula kuwa alielezwa kuwa hati yake haijafika na yeye hakuelewa
kama kuna taratibu hajazikamilisha ili apatiwe hati ingawa alishapatiwa hati za
viwanja vingine viwili alizoomba katika halmshauri hiyo.
Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi katika
halmshauri ya Wilaya ya Serengeti kuhakikisha inawafuatilia waombaji wote wa
ardhi na kuwasaidia kuwaelekeza taratibu zitakazowawezesha
kupata hati zao bila usumbufu wowote.
Alisema, serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais John Pombe Magufuli haitaki kuona wananchi wanasumbuka katika kupatiwe
hati za ardhi kwa kuwa hati hizo ni haki yao na zitawasaidia katika shughuli
zao za kiuchumi hivyo alitaka wahusika wafahamishwe kwa njia ya simu pamoja na
barua kwa lengo la kuweka kumbukumbu sawa.
Aakikagua majalada ya ardhi katika halmshauri
ya Serengeti, Mabula alibaini utunzaji wa majalada usiofuta taratibu na kuamuru
watendaji wa sekta ya ardhi kuhakikisha taratibu zote katika
kushughulikia majalada ya ardhi ikiwemo maelekezo kutoka afisa mmoja
kwenda kwa mwingine yanazingatiwa ili kuepuka ujanja unaoweza kufanywa katika
majalada hayo na kuleta usumbufu kwa waombaji hati.
-----------MWISHO------------
0 comments:
Post a Comment