Kada wa CCM Ndugu Methusela Gwajima, amemshauri Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Mheshimiwa Edward Lowasa Kustaafu rasmi harakati zake za kisiasa na hasa siasa za majukwaa ili kulinda heshima yake.
Gwajima amesema ,Kipigo cha Monduli alichopata ni kibaya mno na ni zaidi ya Kipigo Cha Mbwa Koko kiasi kwamba, kisiasa sasa anatia aibu/Huruma/Simanzi, hivyo anapaswa kusoma alama za nyakati kwani kama ni kuisoma namba hakika hii ya Monduli ni ya kufunga mwaka !!
“Hivi kweli kama umeweza kushindwa kulikomboa Jimbo moja tu tena la Nyumbani kwako, Je utaweza tena kuhimili mchaka mchaka wa nchi nzima ? Kwa hakika busara ya kawaida inakutaka upumzike na ikibidi uachane kabisa na harakati za kisiasa, baki nyumbani walau hata uwe mshauri tu kwa watu watakaohitaji ushauri wako” alisema Gwajima.
Gwajima ambaye ni Mwanasheria kitaaluma amemtaka Lowasa Kuepukana na washauri wabaya waliomzunguka kwani kwa mara nyingine tena wamefanikiwa kumuingiza chaka bure mzee wa watu.
“Nadhani, Mhe. Lowasa amezungukwa na genge la wahuni na wapiga dili ndio maana wanashindwa kumpatia ushauri mzuri unaoendana na umri na heshima yake.
Mhe. Gwajima amewapongeza wagombea wote wa CCM waliofanikiwa kupata ushindi wa kishindo “Hongera sana wanaukonga, Hongera sana wana Monduli, Hakika nyinyi hampangiwi cha kufanya ama kweli wanaukonga na Monnduli sio wa mchezo mchezo”
Mhe. Gwajima amevipongeza vyombo vyote vya dora kwa kusimamia amani na utulivu wakati wote wa kampeni na hatimaye katika zoezi zima la uchaguzi.
Ushindi huu wa CCM katika chaguzi ndogo zilizofanyika jana ,ni ishara kubwa ya imani walionayo wananchi kwa serikali yao chini ya Mhe. Raisi wetu Mpendwa Dr. John Pombe Magufuli katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.
Mhe. Gwajima amepongeza Mh. Raisi Magufuli kwa kufanya mambo makubwa ya wakuwaletea wananchi maendeleo katika sekta zote na mda mfupi sana tangu aingie madarakani.
Mhe. Gwajima Alimpongeza Rais Magufuli kwa ujasiri wake na usimamizi katika kusimamia Ujenzi wa Bomba la mafuta HOIMA –TANGA, Ongezeko Katika makusanyo ya kodi –TRA, Mradi wa STIEGLERS’S GORGE MEGAWATI - 2,100, Mahakama wa rushwa na uhujumu uchumi na Serikali kuhamia makao makuu DODOMA.
Mafanikio ya kuhusu Elimu bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne, Ujenzi wa Ukuta wa kulinda Madini MERERANI, Kufufua Shirika la ndege nchini, Usajili wa kuwatambua rasmi wamachinga 20,000, Huduma bora za tiba kwa watanzania na Mafanikio makubwa katika ujenzi wa miundombinu mfano mzuri ni Flying Over ya Tazara.
Mwisho Mh. GWAJIMA amewaomba watanzania kuendelea kumuunga mkono Raid Magufuli.
0 comments:
Post a Comment