Na George Binagi-Morogoro
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko leo 11 Julai 2018 amekamata madini ya vito aina Rhodilite yanayokadiriwa kuwa tani saba katika nyumba ya mchimbaji na mfanyabiashara mmoja wa madini iliyopo Kata ya Magoweko wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Aliyekamatwa na madini hayo ambayo bado thamani yake haijafahamika ni James Mnene ambaye ni mchimbaji na mmiliki wa kampuni ya madini ya JJ.Mnene & Partiners inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito katika machimbo ya Rubeho wilayani Gairo.
Hata hivyo mfanyabishara huyo amejitetea kwamba alikuwa ametunza madini hayo nyumbani baada ya kukosa soko na kuomba asamehewe kwani yuko tayari kufuata taratibu za biashara ya madini.
Naibu Waziri Biteko (kushoto) akizungumza baada ya kufika nyumbani kwa mfanyabishara huyo (katikati). Mfanyabiashara huyo ametiwa nguvuni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo anatuhumiwa kukweka kulipa mapato ya serikali kwani tangu mwaka 2013 amelipa shilingi laki nne
Madini hayo yakiwa nyumbani kwa mfanyabishara huyo
Nyumba ya mfanyabiashara aliyekutwa amehifadhi madini ya vito wilayani Gairo
0 comments:
Post a Comment