Baadhi ya wananchi wa Kata ya Malambo Mjini Bariadi wakichimba msingi wa wa ujenzi wa madarasa zaidi 40 na mabweni 15 ya Shule ya Sekondari Simiyu ambayo inatarajiwa kuwa shule ya vipaji maalum ya mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Festo Kiswaga (mwenye koleo) akishirikiana na wananchi kwa Kata ya Malambo mjini Bariadi kuchimba msingi wa ujenzi wa madarasa zaidi 40 na mabweni 15 ya Shule ya Sekondari Simiyu ambayo inatarajiwa kuwa shule ya vipaji maalum ya mkoa wa Simiyu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bariadi, Ndg.Nicholuos Kasendamila akishirikiana na wananchi kwa Kata ya Malambo mjini Bariadi kuchimba msingi wa ujenzi wa madarasa zaidi 40 na mabweni 15 ya Shule yaSekondari Simiyu ambayo inatarajiwa kuwa shule ya vipaji maalum ya mkoa wa Simiyu
Na
Stella Kalinga, Simiyu
Wananchi wa Wilaya ya Bariadi
Mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo Festo
Kiswaga wamejitokeza kwa wingi kuchangia nguvu kazi ,
kuchimba msingi wa ujenzi wa madarasa zaidi 40 na mabweni 15 ya Shule ya
Sekondari Simiyu.
Wananchi hao wamejitokeza leo kwa
wingi katika shule ya sekondari ya Simiyu kwa lengo la kuunga jitihada za Mkuu
wa Mkoa wao Anthony Mtaka za kuhakikisha wanakuza na kurudisha heshima ya elimu
Mkoani humo.
Wamesema
kuwa wameguswa na uamuzi wa Serikali wa kuona umuhimu wa kuboresha
mazingira rafiki ya kujifunzia wanafunzi na kujenga shule kubwa ya vipaji
maalum ambayo itakuwa ni msaada na utambulisho wa Mkoa wao.
Yohana
Musa mkazi wa mji wa Bariadi amesema kuwa wamegusa sana na uamuzi wa Serikali
ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wao wa Mkoa Anthony Mtaka wa kuwekeza katika elimu
ambayo itawasaidia watoto wao kufikia malengo waliyojiwekea.
“chini
ya uongozi wa mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya,Mkoa wetu utakuwa na
shule bora itakayochukua idadi kubwa ya wanafunzi walio na vipaji maalum ndani
na nje ya Mkoa wa Simiyu…Alisema Musa.
Mwenyekiti
wa mtaa wa mnara wa voda Songera Magenda amesema kuwa wananchi wake wamekuwa na
muamko wa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo ili kujenga Mkoa wao.
Magenda
amesema kuwa kupitia nguvu kazi za wananchi wake ,ni matumaini yake kuwa ujenzi
wa shule hiyo utaenda kwa kasi na kukamilika mapema mwaka huu ambapo
ukikamilika utatoa fursa kwa wanafunzi wenye vipaji maalum wa Mkoa wa Simiyu
kusoma hapo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amesema endapo shule hiyo
ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000 kwani
inatarajiwa kuwa na mabweni 10 pamoja na vyumba vya madarasa visivyopungua 40.
Kiswaga
amesema kuwa shule hiyo imeanza kujenga kwa jitihata za uongozi wa Mkoa ambao
lengo kuu ni kuona Mkoa wa Simiyu nao unakuwa na shule kubwa,nzuri ya wanafunzi
wa vipaji maalum kama ilivyo mikoa mingine.
Kiswaga
pia ametoa wito kwa wanasimiyu wote wenye mapenzi mema na elimu ,waone umuhimu
wa kujitolea na kuchangia ujenzi wa shule hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati
na kusaidia kundi kubwa na wanafunzi kusoma shuleni hapo.
0 comments:
Post a Comment