METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, May 15, 2018

KIHO YALETA VYUO VIKUU KUNGARISHA KIJIJI CHA RUVU MARWA MKOANI KILIMANJARO

Ni mpango uliounganisha chuo kikuu cha Ohio toka Marekani Na UDOM toka Tanzania.

Kila mwaka wanakutana walimu ( Profs. Na Dr.) Na wanafunzi toka vyuo hivyo Na kukaa kijijini Hapo kwa mwezi mmoja  kuanzia mwaka 2017.

Wakiwa kwenye sherehe ya mapokezi ya wageni hao Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira Amewahimiza wananchi wa Ruvu Marwa kushirikiana Na wageni hao kwa Karibu kuhakikisha miradi wanayoifanya inaisha kwa wakati.

Amepongeza mpango Huu unaowapa wanafunzi mafunzo ya uhalisia Juu ya jamii wanayotakiwa  kuitumikia baada ya masomo yao.

Kwa sasa wameanza Na mradi wa Maji, umeme, uchumi kwa wanawake na mazingira Na upimaji wa Ardhi.

NGO ya KIHO inategemea kuwaleta wadau wengine ili kukifanya Kijiji hicho  kuwa cha mfano. Alisema Ndugu Kateri ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya KIHO.

Wanafunzi hao 10 toka UDOM Na 30 toka OHIO wanategemea kufanya mazoezi ya vitendo kutokana Na utaalamu wao.

"Same is not same"

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com