Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab akizungumza katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama.
...................................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo amewaagiza wakurugenzi wote nchini kujibu hoja za wakaguzi kwa wakati ili kupunguza hati Chafu na Mashaka kwa Halmashauri.
Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na Kamati ya ulinzi na Usalama na Manejimeti ya Mkoa wa shinyanga leo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea miradi yamaendeleo Mkoani hapo.
Amesema Wakurugenzi wanawajibu wa kuhakikisha hoja zote zinazotolewa na wakaguzi zinafanyiwa kazi mapema kwa kutoa majibu stahiki na wakati.
"Kumekuwepo na changamoto kubwa kwa baadhi ya Halmashauri kutotoa majibu ya hoja za wakaguzi zinapotolewana kusababisha kupata hati chafu na zenye mashaka" Amesema
Mhe.Jafo amesema katika hoja za CAG mwaka huu imeonekana kuwa vitabu 379 havijaonekana, hivyo ameziagiza Halmashauri zote nchini kutumia mifumo ya Tehama ili kupunguza ubadhilifu wa mali ya umma na kupunguza mianya ya wizi wa fedha za serikali.
Kuhusu usimamizi wa fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya Miradi ya maendeleo Mhe.Jafo amewaagiza Wakurugenzi kusimamia fedha hizo kea weledi ili miradi hiyo iendane na dhamani ya fedha zilizotolewa nakukamilika kwa wakati.
Amewataka kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo, rasilimali fedha na rasilimali watu ili kuleta maendeleo kwa jamii.
Wakati huo huo, Waziri Jafo amewataka viongozi wote wa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanasimamia suala zima la mauaji ya vikongwe kwa imani za kushirikina kwa kuwa linarudisha nyuma maendeleo na kutoa sura mbaya kwa jamii.
0 comments:
Post a Comment