Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza na wataalamu wa sekta ya kazi na
ajira wakati wa mkutano uliowakutanisha Jijini Dar es Salaam kwa ajili
ya kupitia na kujadili ajenda mbalimbali zinazohusu sekta hiyo.
Sehemu ya
Wataalamu wa Sekta ya Kazi na Ajira kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia mada
zilizokuwa zikiwasilisha katika mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es
Salaam.
Mwakilishi wa
sekretarieti ya SADC, Bw. Maxwell Parakokwa (kushuto) akifafanua jambo
wakati wa mkutano huo uliowakutanisha wataalamu wa utatu wa sekta ya
kazi na ajira Novemba 20, 2019 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.
Andrew Massawe na Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu
SADC, Bi. Duduzile Simelane (katikati).
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilisha kuhusu sekta ya Kazi na Ajira.
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew
Massawe (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii
na Rasilimali Watu SADC, Bi. Duduzile Simelane na Mwakilishi wa
sekretarieti ya SADC, Bw. Maxwell Parakokwa wakati wa mkutano
uliowakutanisha wataalamu wa sekta ya kazi na ajira.
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew
Massawe akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wazee,
Wanawake na Watoto Zanzibar Bi. Fatma Bilali wakati wa mkutano wa
wataalamu wa sekta ya kazi na ajira.
Mkurugenzi wa
Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Willington
Chibebe akieleza jambo kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe wakati wa mkutano wa
wataalamu wa sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Kazi kutoka Afrika Kusini Bw. Virgil Seafield akichangia mada wakati wa mkutano huo.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
0 comments:
Post a Comment