Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Christopher Ole Sendeka akizungumza na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba Ofisini kwake Mkoani Njombe hivi karibuni. Wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Ndg Jackson Saitabahu, Mkurugenzi wa Maendeleo ya mazao (NFRA) Ndg Mikalu Mapunda na Frank Makonjo Meneja NFRA Kanda ya Makambako. Picha Na Mathias Canal, NFRA.
Na Mathias Canal, NFRA
Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umetakiwa kuwasaidia wakulima nchini
kutengeneza soko la mazao mbalimbali wanayozalisha hususani mahindi ili kupata
soko la kuridhisha nje ya nchi.
Jukumu
hilo endapo kama NFRA italifanya la kutafuta na kuboresha masoko ya mazao nje
ya nchi linatazamiwa Kuimarisha soko na kuchangamsha bei jambo ambalo
litawanufaisha wakulima kote nchini hivyo kuona umuhimu wa nguvu kazi
wanazotumia katika kilimo.
Mwito
huo ulitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Christopher Ole
Sendeka wakati akizungumza na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba Ofisini kwake Mkoani Njombe.
Katika
kuimarisha uhifadhi mahususi wa maeneo ya kuhifadhia chakula tayari NFRA
imezindua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa ambapo katika Halmashauri ya
Mji wa Makambako Mkoani Njombe vitajengwa Vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani
20,000 sambamba na Tani 20,000 za maghala hivyo kufanya uwezo wa kuhifadhi kuwa
tani 79,000 kutoka uwezo wa sasa wa Tani 39,000.
Sambamba
na hayo pia Mhe Ole Sendeka amewaomba wananchi kote nchini kuanzisha utamaduni
mahususi wa kununua chakula na kuhifadhi kwani kufanya hivyo itatoa urahisi wa
kuuzwa kwa ziada inayosalia.
Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula unamiliki maghala ya kuhifadhi nafaka 34 kote
nchini yenye uwezo wa jumla ya Tani 251,000.
Aidha,
Uwezo huu wa sasa wa maghala hautoshelezi mahitaji ya dharula ya chakula kwa
mfululizo wa miezi mitatu kwa akiba isiyo pungua Tani 700,000, hivyo kupelekea
uhitaji wa kuongeza uwezo wa uhifadhi. Hivyo, mradi wa ujenzi wa maghala na
vihenge vya kisasa ambao ulizinduliwa juzi 21 Aprili 2018 na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb), umeanzishwa ili
kukidhi lengo la Wakala kuhifadhi chakula kisichopungua Tani 700,000.
Naye
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi
Vumilia L. Zikankuba alimuhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe kuwa Wakala
umejipanga vyema kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa
serikali inakuwa na akiba ya kutosha ya mazao ili kukidhi matakwa ya majukumu
ya msingi ya kuwahudumia wananchi kwa mujibu wa dira ya kuwa taasisi yenye
uwezo wa kukabiliana na upungufu wa chakula kwa wakati ifikapo mwaka 2020.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment