Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini
Vyamhokya katikati akiongoza kuimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa
kikao na wanahabari mjini Iringa .
..................................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
WAKATI maadhimisho ya siku
ya wafanyakazi duniani kwa
nchini Tanzania yaliyoandaliwa na shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) yakitaraji
kufanyika mkoani Iringa
kitaifa mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina
Masenza amesema mkoa
wa Iringa kuwa mwenyeji wa
mei mosi ni heshima
kubwa katika Taifa .
Akizungumza na wanahabari
leo ofisini kwake kuhusiana na maandalizi ya Mei
Mosi Kitaifa alisema
kuwa mkoa wa
Iringa umeteuliwa kuwa mwenyeji
wa maadhimisho hayo ambapo mgeni
rasmi atakuwa ni Rais
Dkt John Magufuli .
Alisema kuwa
katika maadhimisho hayo ya Mei
Mosi kitaifa kauli
mbiu ni Kuunganishwa kwa mifuko ya
hifadhi ya jamii kulenge kuboresha mafao ya wafanyakazi na
kuwa kupitia maadhimisho hayo
wakazi wa mkoa wa
Iringa na wafanyabiashara watapata
fursa kubwa ya
kujitangaza pamoja na kuonyesha shughuli zao.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akila kiapo mbele ya Rais Dkt Jonh Magufuli pindi alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa |
Katika maadhimisho hayo
ambayo kilele chake
kitafanyika uwanja wa Samora
mjini Iringa kabla ya kilele
kutakuwa na michezo mbali mbali
kama mpira wa miguu, kuvuta kamba ,bonanza la michezo
tofauti ,mpira wa pete ambayo
yote yameanza toka April 17 hadi
April 30 mwaka huu .
Hata hivyo mkuu
huyo wa mkoa wa Iringa mwenyeji
wa Mei
mosi kitaifa mwaka 2018
Bi Amina Masenza alisema
sherehe hizo zitahusisha maonyesho
ya shughuli ,huduma na bidhaa mbali mbali za wafanyakazi ,taasisi za
umma na binafsi ,wawekezaji na wajasiliamali zitakazofanyika uwanja
wa Kichangani Kihesa mjini
hapa .
Hata hivyo alisema
kwa ajili ya kuufanya mkoa wa
Iringa uzidi kuwa fursa kwa wageni
kutembelea vivutio vya
utalii kama hifadhi ya Ruaha
na vingine serikali imekaa na
wafanyabiashara wa nyumba
za kulala wageni na Hoteli
ili kuepuka kutumia mei
mosi kupandisha gharama
za vyumba kwa wageni .
Bi Masenza amewataka
wananchi wa mkoa wa
Iringa na wafanyakazi
wote kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais
wetu mpendwa wetu Dkt John
Magufuli .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment