METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 29, 2020

DKT MABULA: ITUMIENI MICHEZO KUIMARISHA AFYA, KUONGEZA UFAHAMU


Wanafunzi na walimu wa shule za msingi na sekondari kwa manispaa ya Ilemela wametakiwa kutumia michezo kwaajili ya kuimarisha afya zao dhidi ya magonjwa na kuongeza ufahamu kwa watoto hivyo kuchochea ufaulu.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula katika viwanja vya shule ya msingi Sabasaba wakati akifungua mashindano ya MWAOMI Inter School Sports Competition yanayohusisha shule za sekondari na msingi za ndani ya manispaa hiyo yanayotegemewa kufika tamati Septemba 19, ambapo amesema kuwa Serikali imedhamiria kukuza michezo kwa kushirikiana na wadau kwa kuhakikisha wanajenga na kuimarisha miundombinu kwaajili ya michezo hivyo kuwaomba kuitumia kwa kuimarisha afya za watoto na kuwa kishawishi cha kuongea ufaulu katika masomo yao kwa kutenga muda wa michezo na kujifunza

‘..  Mlezi wa wilaya ya Ilemela na Mkamu wa Rais Mhe Samia Suluhu anatuhimiza kufanya mazoezi, Na kama mnavyojua michezo ni sehemu ya mazoezi, Tuitumie kwaajili ya kuimarisha afya zetu ..’ Alisema

Aidha Dkt Mabula akatumia fursa hiyo kuipongeza manispaa ya Ilemela chini ya mkurugenzi wake Ndugu John Wanga kwa kukubali viwanja vya shule zake kutumika kwa shughuli za michezo sanjari na kuwakaribisha wadau wa maendeleo na kuwaahidi ushirikiano katika kuhahakisha sekta ya michezo inaendelezwa.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Mratibu wa shirika la MWAOMI Ndugu Fredrick Eliachim Rubinda mbali na kuelezea historia ya mashindano hayo akabainisha faida mbalimbali watakazopata washiriki ikiwemo kujenga afya za miili yao, kuimarisha ubongo, kuwaepusha na kujiingiza katika matendo ya uvunjifu wa sheria na yasiyofaa kama uasherati na matumizi ya dawa ya kulevya.

Nae afisa michezo wa manispaa ya Ilemela Mwalimu Bahati Sosho Kizito akasema kuwa licha ya wilaya yake kuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na michezo bado inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya michezo hivyo kuwaomba wadau kuzidi kujitokeza kupambana na changamoto hiyo.

Akihitimisha moja ya wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo, Salma Yahya kutoka shule ya sekondari Lumala akashukuru kwa uwepo wa michezo hiyo kwani ni muda mrefu wamekuwa na likizo ya kimichezo kutokana na ugonjwa wa homa ya mafua makali Covid-19.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com