Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa
Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC aliyemaliza muda wake kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda umefanyika hapa
Luanda, leo tarehe 24 Aprili, 2018.
Mkutano huu
umeitishwa baada ya mashauriano kati ya Mheshimiwa Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais
wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC na Mhe. João Lourenço, Rais wa Angola na Mwenyekiti wa
Asasi ya Ushirikino ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC
Mkutano huu
umetanguliwa na kikao cha Mawaziri ambacho kilifanyika jana tarehe 23 April
2018.
Mkutano huu
ulihusisha nchi wanachama sita tu wa SADC Double Troika na Viongozi wafuatao
walihudhuria, Mhe. Dkt. Cyril
Ramaphosa, Rais wa Afrika
Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe.
João Lourenço , Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya
Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and
Security Cooperation),Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia na Makamu
Mwenyekiti wa SADC Organ, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland na Mwenyekiti wa Summit anayetoka;
Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange, Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho walialikwa na
walihudhuria.
Mkutano huu utapitia na
kujadili ajenda zifuatazo:-
(i)
Hali ya siasa na
usalama katika Falme ya Lesotho;
(ii)
Hali ya siasa ulinzi na usalama katika Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo;
(iii) Hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Madagascar;
na
(iv) Masuala ya demokrasia katika kanda ( Consolidation of Democracy in the region)
KUHUSU HALI YA SIASA,
ULINZI NA USALAMA NCHINI LESOHO:-
(i)
Mkutano huu
umevitaka Vyama vyote vya Siasa kulipa
uzito suala la Mjadala wa Kisiasa na Mchakato wa Mageuzi ya Kisekta na
kushiriki kikamilifu kwenye michakato yote ili kupata suluhisho la kudumu
katika changamoto za kiusalama na kisiasa;
(ii)
Pia Mkutano huu
umeitaka Serikali ya Lesotho na wadau wengine kukamilisha mjadala wa kitaifa
ifikapo mwezi Juni, 2018 na kutoa taarifa kwenye kikao kijacho cha kawaida cha
Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ambacho kimepangwa kufanyika Augosti, 2018;
(iii)
Pia Misheni ya
Ulinzi nchini Lesotho (SADC Preventive Mission in the Kingdom of Lesotho -
SAPMIL ) imeongezewa muda kwa kipindi kingine cha miezi sita kuanzia Mei 20,
2018.
KUHUSU HALI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO (DRC)
Nchi wanachama zitaombwa kuisaidia Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) kwenye kipindi hiki wanachoelekea kwenye
Uchaguzi Mkuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa uchaguzi huu unafanyika katika
mazingira ya amani.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huu ulitumia
fursa hiyo kuomba nchi wanachama wa SADC kumuunga mkono Mheshimiwa Stephen
Maselle ( Mb), ambaye anawania nafasi ya
Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (
Deputy President of the Pan African Parliament).
24 APRILI, 2018
0 comments:
Post a Comment