Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Mavunde * amefungua Mkutano wa Bunge kivuli la Vijana chini ya Umoja wa Mataifa kwa niaba ya *Mh Samia Suluh Hassan* kwa kuwataka Vijana kutumia teknolojia kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili Vijana duniani kote.
Mavunde ameyasema hayo leo asubuhi mapema katika ukumbi wa *TREASURY SQUARE* mjini Dodoma wakati akifungua mkutano huo unaojumuisha Vijana kutoka Mataifa 12 duniani kwa kuwataka Vijana kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii na kuwa Wabunifu katika kubuni njia za kutatua changamoto mbalimbali katika jamii kwa kufanya matumizi sahihi ya teknolojia.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa *YUNA TANZANIA* Bi Jacqueline Kamwau amesema mkutano huo ni wa siku 5 na baadaye wataandaa maazimo na kuwasilisha serikalini na kwa wadau wa Vijana ili kutengeneza mpango endelevu wa maendeleo ya Vijana.
0 comments:
Post a Comment