Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya
uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro,
Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo
hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo
ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3)
kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Mwezeshaji na Afisa Habari kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah akiwasilisha mada kuhusu mtindo wa uandishi wa habari katika tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Na
Mwandishi Wetu, MOROGORO
MAAFISA Habari na
Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa
kuacha kufungia katika makabati na makabrasha taarifa chanya za utekelezaji wa
mikakati, miradi na programu mbalimbali za Serikali na badala yake watangaze
mafanikio hayo kwa umma.
Hayo yamesemwa jana
(Jumanne Machi 20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu mwongozo
wa uandishi wa habari za tovuti kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za
Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Thadeus alisema
Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri
mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika
maeneo hayo watangaze mafaniko hayo badala ya kusubiri maswali na hoja
mbalimbali za wananchi wakihoji katika kupata uelewa kuhusu miradi hiyo.
“Maafisa Habari,
msifungie taarifa katika makabati yenu toeni taarifa kwa Umma, wananchi
wanapenda kufahamu nini kinafanywa na Serikali yao hivyo jukumu la Afisa Habari
ni kupiga picha kuandaa taarifa na wekeni vielelezo hivyo katika tovuti zenu
ili kujibu hoja za wananchi” alisema Thadeus.
Aidha, alisema ni
wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha kuwa wanaweza taarifa mpya
kila wakati ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya msingi ya wananchi ambao
wamekuwa wakitumia muda mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma mbalimbali
zinazotolewa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Akifafanua zaidi
alisema Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali
nchini ndiyo wataalamu wa masuala ya Mawasiliano katika maeneo yao ya kazi,
hivyo wana wajibu wa kutoa ushauri kwa viongozi wao wa kazi kwa ajili ya kutoa
ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu hoja mbalimbali zinazoulizwa na kujitolea
majibu kwa wakati.
Aliongeza kuwa matumizi
ya tovuti ndiyo njia ya haraka zaidi ya kurahisisha mfumo wa utoaji wa habari
na taarifa mbalimbali za Halmashaauri na Mikoa, hivyo ni wajibu wa Maafisa
Habari na Mawasiliano kuwa mabalozi ili kuhakikisha kunakuwepo na daraja la
mawasiliano baina ya Serikali na wananchi katika kupata suluhu ya masuala
mbalimbali ikiwemo migogoro inayotokea mara kwa mara.
Kwa upande wake, Kiongozi
wa Timu ya Utawala Bora kutoka PS3, Dkt. Peter Kilima alisema uboreshaji wa
tovuti ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa dhana halisi ya utawala bora hivyo ni
wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri nchini
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa zinazozingatia muda na mahitaji
yaliyopo.
Aliongeza ni wajibu wa
Maafisa Habari na Mawasiliano kuzingatia mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa
habari katika tovuti za Serikali katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini
kwa kuwa wananchi wana matarajio makubwa na Serikali yao katika kuwapatia
huduma mbalimbali.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment