Pichani:Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng'anzi
Pichani: Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi ambae ni mchungaji wa kanisa la Zumaridi
MWANZA
Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi ambae ni mchungaji wa kanisa la Zumaridi kwa tuhuma za usafirishaji haramu wa binadamu 149 wakiwemo watoto wenye umri kati ya miaka 4 hadi 17.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng'anzi amesema, polisi walipokea amri ya mahakama ya mwanzo Mkuyuni kumtafuta na kumkamata mzazi wa mtoto Samir Abbas aliyetakiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kwenda shule kupata haki yake ya msingi ya kupata elimu ndipo polisi walipobaini mzazi huyo pamaoja na mtoto wake kuwepo nyumbani kwa mchungaji huyo anayejiita mfalme, na baada ya kufika nyumbani hapo ndipo walipowakuta watu wengine 149 kati yao wakiwemo watoto 24.
aidha kamanda Ng'anzi amesema upelelezi utakapokamilika wa tuhuma zinzazomkabili mchungaji huyo atafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
katika tukio lingine kamanda Ng'anzi amesema jeshi la polisi limetekeleza maelekezo ya mwendesha mashtaka Taifa DPP ya kuwaachia watuhumiwa 36 wa makosa ya ugaidi ambao wamekidhi masharti ya dhamana na wataendelea kuwaachia wengine watakaokidhi masharti hayo
0 comments:
Post a Comment