Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .kwaniaba ya Raisi John
Pombe Magufuli leo March/21/2018 amesaini mkataba wa Makubaliano ya
kulifanya Bara la Afrika Kuwa eneo hururu la Biashara . Utiaji saini huo
umefanyika Jijini Kigali Rwanda. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepongeza makubaliano yaliyofikiwa
na nchi za Afrika za kulifanya bara hilo kuwa eneo huru kibiashara.
Majaliwa aliyasema baada ya kumaliza kusaini mkataba wa
nchi za Afrika kuhusu mkataba huo akimwakilisha Rais John Magufuli Jijini
Kigali ambapo alisema Tanzania imeajiandaa vya kutosha kutekeleza mkataba
huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali , Waziri Mkuu
alisema Tanzania itahakikisha mkataba huo unatelekezwa bila kuathiri huduma
zinazozalishwa ndani.
Alisema Tanzania itahakikisha mikataba mitatu ambayo imesainiwa
inatekelezwa bila kuathiri uzalishaji na sera za ndani.
Mikataba iliyosaioniwa na mataifa hayo 50 ya Bara la
Afrika ni pamoja na mkataba wa kulifanya bara la Afrika kuwa eneo huru la
biashara, Itifaki ya kisheria ya utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwamo
uhuru wa makazi, haki ya kuishi na kufanyakazi popote bila vikwazo wala vizuizi
vyoyote.
Azimio la tatu ni Azimio la Kigali ambalo limejumuisha mawazo ya
uanzishwaji wa mchakato huo.
“Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika (AU), Paul Kagame kwa kutilia maanani suala hili hadi kufikia
hatua hii ya kusaini mkataba.
“Tanzania kama wadau wakuu wa mkataba huu tunakwenda kujipanga
kuhakikisha mkataba huu unatekelezwa bila kusababisha vikwazo vyovyote.
“Hata hivyo tunakwenda kupeleka baadhi ya masuala haya katika
vikao vya Baraza la mawaziri ili kuangalia sheria zetu zisije kuwa kikwazo
katika utekelezaji wa mkataba huu.
“Kwa mfano Tanzania tunayo sera ya viwanda, lazima tuangalie ili
tusije kuruhusu bidhaa kuingia nchini mwetu na kuathiri biashara na bidhaa zetu
za ndani.
Vile vile katika uhuru wa biashara ya anga ambapo Tanzania bado
tuna ndege chache ili tusije kuruhusu kiholela, l;azima tuwe waangalifu katika
hilo.
“Aidha Tanzania tumeruhusu maeneo ya kuzalisha bidhaa, kwa hiyo
lazima tuwe makini ili tusije kuruhusu na kuharibu mwenendo wa kiuchumi.
Awali akihutubia katika ufunguzi wa sherehe hizo, Rais wa
Rwanda, Paul Kagame aliyataja maeneo makuu ambayo mkataba huo umeangazia kuwa
ni pamoja na eneo huru la biashara ya anga, miundombinu ya reli na barabara
ambayo itaziunganisha nchi za Afrika kuwasiliana kwa urahisi.
Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), alisema
mkataba huo unatoa nafasi maalum ya Ukanda wa Afrika kujali utu,
kumnufaisha mkulima, mfanyabiashara na wabia wengine wa maendeleo kuja kutafuta
fursa Afrika.
“Azimio hili linatoa nafasi kununu na kuuza bidhaa sambamba na
kupata wabia duniani kote, biashara huru itatuweka pamoja na muafaka wa Afrika
tutakayo” alisema Rais Kagame.
Mkataba huo ulisainiwa jana baada ya vikao vya maadalizi
vilivyohusisha timu za wataalam na mawaziri wa biashara na mambo ya nje ya nchi
zinazounda Umoja huo.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 50 wanachama wa AU ambao walisaini
mkataba huo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment