Na Mwandishi Wetu, Tabora
MBUNGE
wa Jimbo la Ushetu Wilayani Kahama Mhe. Emmanuel Cherehani ameshiriki mkutano
mkuu wa nne wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo kilichopo Mkoani Tabora
akimuwakilisha Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe.
Amesema
katika kipindi hichi cha kuelekea kwenye manunuzi ni muhimu wote wanaohusika na
mnyororo wa zao la tumbaku kuhakikisha bei inakuwa nzuri, kuteua madaraja kwa usahihi wa sokoni na kutatua
changamoto zinazowakabili wakulima ili mkulima aweze kurejesha mikopo na
kuinuka kiuchumi.
Cherahani
ametoa rai hiyo wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mkoani Tabora
leo tarehe 26 Februari 2022 na kuhudhuriwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa
Bodi ya Tumbaku Tanzania, wanunuzi wa Tumbaku, Taasisi za Fedha pamoja na
wawakilishi wa vyama vikuu vinavyolima Tumbaku.
Mbunge
Cherehani amewataka viongozi kuhakikisha wanasimamia malipo ya wakulima ili
waweze kulipwa kwa wakati jambo litakalowafanya waweze kufanya maandalizi ya
mashamba kwa ajili ya msimu unaofuata kwa wakati.
Katika
hatua nyingine Mhe Cherehani amempongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea kutatua changamoto za wakulima.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment