Katika ziara ya ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefanya Mkutano wa ndani na mamia ya wanachama wa CCM katika Kata ya Kazuramimba ambapo amepokea pongezi za wananchi kwenda kwa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais na Mwenyekiti wa CCM kwa kazi nzuri ya ujenzi wa Taifa na amempokea baadhi ya changamoto za wananchi wa Kata ya Kazuramimba ikiwemo huduma za afya na elimu.
Ndg. Polepole amewahakikishia wananchi wa Kata ya Kazuramimba na Wilaya ya uvinza kuwa CCM imeshadhamiria kushughulika na shida za watu hivyo changamoto za maeneo yao zitapatiwa ufumbuzi kwa wakati na hakika.
*Nawahakikishia utolewaji wa Huduma za afya na hasa Uzazi, Mama na Mtoto ni kipaumbele cha Serikali ya CCM, nitakuwa balozi wenu na kuwasemea ili miundo mbinu hii ikamilike mapema zaidi*
amesema Ndg. Polepole
Wakati huo uo Ndg. Polepole ametembelea Kata ya Nguruka na kufanya kikao cha ndani na Wanachama wa CCM na amewahakikishia mpango wa Serikali ya CCM kuwaletea umeme wananchi wa Nguruka ni wa hakika hivyo wananchi waendelee kuunga mkono Serikali ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Njiani ndugu Polepole ametembelea ujenzi wa Ofisi kubwa ya CCM Wilaya ya Kaliua inayojengwa na wanachama na akaahidi kuwashirikisha viongozi wa CCM Taifa ili nao waunge mkono jitihada hizi za kuigwa
Huu ni muendelezo wa ziara za ujenzi wa Chama ili kuuhisha dhana ya CCM MPYA TANZANIA, CCM, chama cha watu na kinachoshughulika na shida za wananchi.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
0 comments:
Post a Comment