Na Bashir Nkoromo, Kigamboni
Wanawake wajasriliamali wametakiwa kutengeneza au kuuza bidhaa zenya ubora wa viwango vinavokubalika ili kuvutia wateja kununua bidhaa zao na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila, Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Dege katika Kata hiyo Angela alisema mbali na na bidhaa bora kuhamasisha wanunuzi na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi boa bidhaa hizo zinaweza kumudu ushindani katika soko.
Alivishauri vikundi vya wanawake wajasiriamali kwenda kuomba mikopo kwenye Benki ya Wanawake Tanzania ambayo alisema ni benki yenye mikopo ya riba nafuu.
Uzinduzi wa Jukwaa hilo ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yatafanyika mapema mwezi huu.
Wanawake wa vikundi vya Wajasiriamali wakiandamana kutoka kwenye Ofisi yao kwenda kwenye uwanja wa Dege, kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Dar es Salaam, leo
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kaya ya Somangila, Kigamboni Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa uhuru FM Angel Akilimali (kulia) akiwa na baadhi ya Viongozi wa Jukwaa hilo wakati wakipokea maandamano ya Wanawake wajasiriliamali kwenye uzinduzi wa Jukwaa hilo, leo
Viongozi wa Vikundi mbalimbali vya Wanawake Wajasili na Jukwaa la Wanawake wakiwa tayari kupokea maandamano ya wanawake Wajasiriamali. Kushoto ni Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM angel Akilimali akipunga mikono
Viongozi wakimwayamwaya kupokea maandamano hayo
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akisoma moja ya mabango waliyokuwa nayo Wanawake Wajasiliamali walipowasili Uwanjani kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila.
Diwani wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Francis Chihi (kulia) akionyesha umahiri wa kusakata muziki pamoja na Kinamama wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata hiyo, leo
Mwanamke Mjasiriamali wa kutengeneza vifaa vya ujenzi Amina Zakumera (kushoto) akimpatia maelezo ya utaalam wake Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali (Wapili kulia) alipokuwa akikagua bidhaa za Wanawake wajasiriamali wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Wanawake wa Kata ya somangila, Kigamboni, leo
Angel Akilimali akipata maelezo kuhusu bidhaa za mwanamke Mjarismali Winifrida Jafari (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somanga, Kigamboni leo. Wapili kushoto ni Mjasiriamali Joha Amour wa Joha Fashion.
Angel Akilimali akitazama mkeka uliotengenezwa na Mwanamke Mjasiriamali Jawa Maulidi (kushoto)
Friday, March 2, 2018
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa upinzani, Kizza Besigye akisindikizwa na maofisa wa gereza la Luzira alikokuwa akishikiliwa Kiongozi w...
-
Na Munir Shemweta, WANMM Serengeti Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula ameagiza zoezi...
-
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akijiandaa kukata keki katika katika sherehe ya kuwapongeza...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
Kuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu, kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto ...
Powered by Blogger.











0 comments:
Post a Comment