METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 16, 2018

MBUNGE WA ILEMELA AKABIDHI MATOFALI SHULE YA MSINGI NSUMBA

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula leo amekabidhi jumla ya tofali Elfu Moja na Mia Tano kwa shule ya msingi Nsumba iliyopo kata ya Kiseke kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika shule hiyo kuunga mkono Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli ya kutoa elimu bure

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa amedhamiria kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kusaidia watoto wanaosoma katika shule za jimbo lake waweze kupata elimu bora na yenye gharama nafuu  itakayosaidia kwenda sambamba na Sera ya nchi ya kuwa na uchumi wa viwanda kwa kuzalisha wataalamu watakaotumika katika kufikia malengo  hayo ya nchi.

‘… Wote tunajua kuwa sera ya nchi yetu kwa sasa ni kuwa na nchi yenye uchumi wa viwanda, Najua hatuwezi kufika huko bila ya kuwa na wataalamu wenye weredi kulingana na mahitaji kama hatutoboresha mazingira ya utoaji wa elimu tuliyonayo ili yaweze kutuzalishia wataalamu wa kuendesha nchi yetu kuyafikia malengo tuliyojiwekea …’ Alisema.

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka viongozi wengine na wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya jimbo lake kujitokeza na  kuunga mkono jitihada hizo ili kumaliza kabisa kero na changamoto zinazokabili shule za jimbo la Ilemela.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nsumba, Bi Yombo Manyama amemshukuru mbunge huyo wa jimbo la Ilemela kwa msaada alioutoa wa tofali utakaosaidia ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa ili kupunguza shida ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabiri ya upungufu wa madarasa kufuatia ongezeko lilijitokeza mara baada ya serikali kuanzisha Sera ya Elimu bure iliyofanya wananchi wanyonge na masikini waliokuwa hawana uwezo wa kwenda shule kuanza kunufaika huku akibainisha kuwa zaidi ya watoto mia tatu wanategemewa kunufaika mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.

Wakati huo huo Mbunge huyo ametembelea na kukagua muendelezo wa mradi wa utengenezaji wa tofali unaofanywa na taasisi ya The Angeline Foundation kwaajili ya kusaidia taasisi mbalimbali za umma zenye uhitaji ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi kwa haraka na karibu

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijuenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
16.02.2018

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com