METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, February 13, 2018

ASAS YA METDO TANZANIA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA USIMAMIZI MAKINI WA SEKTA YA MADINI

ASASI YA MINING AND ENVIRONMENTAL TRANSFORMATION FOR DEVELOPMENT ORGANIZATION  METDO Tanzania Inampongeza Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg JOHN POMBE MAGUFULI  kwa jitihada za kuhakikisha Watanzania wananufaika na Madini. 

Akizingumza na uwongozi wa wachimbaji wadogo na uwongozi wa kijiji cha Kakola wilaya ya Kahama, Mkurugenzi wa METDO Tanzania Ashraph Omary Katika  kikao alichokaa na uwongozi huo wanamshukuru sana Mhe Rais JOHN POMBE MAGUFULI kwa kutambua mchango uliopo kwenye Madini na kuiyomba sana METDO  Tanzania kuwapatia Elimu ya usalama kazini ili kuepusha vifo vya mala kwa mala vinavyotokea sehemu za wachimbaji wadogo.

"Sisi wachimbaji wadogo tunamchango mkubwa sana iwapo tutapewa Elimu na kutambua wajibu wetu katika Shughuli tunazofanya ili tuweze kuijenga Nchi,Tunadharaulika wachimbaji wadogo kwa sababu sijui tunaonekana hatujasoma ,Ila kiongozi sisi tukisimamiwa vizuri tunamchango mkubwa  sana katika Nchi yetu,nyie mnakuja inapotokea Ajali "Alisema mmoja wa Wachimbaji katika kikao

Kwa muda mrefu sana wachimbaji wadogo wamekuwa hawapati vema sana Elimu ya Kodi na kutambua wajibu wao.

Kwa idadi iliyopo Tanzania ya wachimbaji wadogo wakilipa  kwa kuzingatia sheria ,Tanzania itaingiza pesa nyingi kwani kinachoitajika ni kuweka utaratibu nzuri kwa kila Halmashauli zote Tanzania zenye Wachimbaji ili kuwapatia Elimu na utaratibu Maafisa wa TRA, MADINI, Mazingira na Halmashauli  husika ili waweze kufanya kazi ya kukusanya kodi na elimu ya Mazingira kwa wachimbaji sehemu za wachimbaji kwa Pamoja.

 Mkurugenzi wa METDO Tanzania Ndg Ashraph Omary kaiyomba Serikali ilichukulie kwa umakini mkubwa  sana swala la Wachimbaji wadogo kuwa na vifaa vya Usalama ,nakupewa elimu ya usalama kazini katika sehem zao za kazi, Ili kupunguza matukio ya ajali zinazoendelea na kupunguza Rasilimali watu wanaopoteza maisha.

TUYATUNZE MAZINGIRA YATUTUNZE 

TUTUMIE RASILIMALI  ZETU KWA AJILI YA KUINUA UCHUMI WA TANZANIA NA KUIJENGA TANZANIA
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com