METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 9, 2018

DKT MWIGULU AAGIZA PIKIPIKI ZILIZOSHIKILIWA MUDA MREFU KUACHIWA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa muda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa muda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Dk Mwigulu amesema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya, na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazitatua haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.

"wapeni masomo wamekosea wapi walekezeni na waliowabishi waelekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunawo, tutumie huu mkono wakutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu" alisema Dk Mwigulu

Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila napopita kita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com