METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 9, 2018

DKT ANGELINE MABULA AFUNGUA MAFUNZO YA UONGEZAJI WA THAMANI ZAO LA MUHOGO

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula leo amefungua mafunzo ya siku tatu kwa wakulima wa zao la muhogo kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza na wilaya jirani za Chato na Biharamulo yaliyoendeshwa na wataalamu kutoka wizara ya Kilimo kupitia taasisi ya Chinga Respect  Company Limited ya  Ilemela  mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mwanza hoteli

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya mbunge huyo, Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela Ndugu Michael Goyele amesema kuwa mbunge wa jimbo la Ilemela anatambua changamoto kubwa zinazoikabili sekta ya kilimo huku akipongeza serikali kwa jitihada zinazochukuliwa kuhakikisha wanasaidia kupunguza changamoto hizo ikiwemo utoaji wa mbolea, zana za kilimo na elimu ya kilimo bora na cha kisasa chenye tija na faida kubwa kupitia tafiti zinazofanywa na wataalamu wake ambapo amesema

‘… Natambua changamoto kubwa zinazoikabili sekta hii ya kilimo na naipongeza Serikali kwa jitihada inazozichukua katika kupambana na changamoto hizi zinazokwamisha tija na thamani ya kilimo cha zao la muhogo kwa wananchi wenzetu lakini niwahakikishie sisi kama viongozi wenu tutaendelea kushirikiana kuhakikisha tunaboresha sekta ya kilimo kwa kukifanya kuwa bora zaidi na cha kisasa …’

Aidha Mhe Angeline Mabula ameasa taasisi za Serikali zinazojihusisha na tafiti za kilimo na wataalamu wa ngazi ya mkoa, wilaya na kata kufika vijijini kusikiliza na kuzipatia  ufumbuzi adha  na kero zinawakabili wakulima

Kwa upande wake Bi Mwanaidi Kiya mtaalamu wa hifadhi ya mazao kutoka wizara ya kilimo mbali na kufafanua juu ya jitihada zinazofanywa na Serikali katika kukuza na kuliongezea thamani zao la muhogo amewaasa wakulima waliojitokeza katika mafunzo hayo kulipa kipaumbele zao hilo linalostamili ukame na hali ya hewa ya mkoa wa Mwanza ili kuongeza upatikanaji wa chakula na kujiongezea kipato

Kwa upande wake mmoja wa wanamafunzo kutoka kata ya Buswelu Ndugu Ernest Mashinene ameshukuru uwepo wa mafunzo hayo, huku akiamini kupata ufumbuzi wa changamoto ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili ya  magonjwa yanayokabili zao la muhogo kutoka kwa wataalamu wa wizara ya kilimo watakaotoa mafunzo ya uongezaji wa thamani kwa zao la muhogo

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
08.02.2018

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com