METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, January 27, 2018

WADAU WA MAENDELEO KARIBUNI ILEMELA

Mbunge wa Jimbo la Ilemela amewakaribisha wadau wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika Jimbo lake ikiwa ni mkakati wake wakuhakikisha anaboresha maisha ya wananchi wake

Kauli hiyo ameitoa ofisi za halmashauri ya manispaa ya Ilemela alipokaribisha Ugeni wa wataalamu wa macho kutoka nchini Ujerumani waliopo mkoani Mwanza kituo cha Mtakatifu Clea cha Kanisa Katoriki kusaidia utoaji wa huduma za macho na kufundisha wataalamu wengine juu ya huduma hiyo ambapo ameshukuru kwa ujio wao na kuwahakikishia ushirikiano ndani ya Jimbo lake

'... Napenda kuwakaribisha sana Ilemela na mmechagua sehemu sahihi kabisa kwakuwa wapo wananchi wangu wengi wenye uhitaji wa huduma yenu na hasa wa maeneo ya nje kidogo ya mji, Hivyo niwahakikishie ushirikiano na utayari katika kusaidia watu wetu ...' Alisema

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewatoa hofu na kuwakaribisha wadau wengine wowote wa maendeleo na wawekezaji kuja Ilemela kwani ni sehemu salama na yenye fursa nyingi

Nae kiongozi wa msafara wa Ugeni huo  Padre Dkt Xavery Kazimoto Komba amesema kuwa lengo lao kuu ni kuanzisha kituo cha kisasa cha utoaji wa huduma ya macho na kufundisha elimu hiyo wataalamu wazawa ili kuwajengea uwezo zaidi pamoja na kuahidi kutoa gari la kubebea wagonjwa kwa Jimbo la Ilemela ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu

Akihitimisha Diwani wa kata ya Kawekamo Mhe Japhes Rwehumbiza aliyeambatana na Mbunge wa Jimbo la Ilemela amesema kuwa ataendelea kushirikiana na Mbunge huyo katika shughuli za maendeleo huku Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Daniel Batare akiwahakikishia utayari na ushirikiano katika kufanikisha adhma hiyo

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
27.01.2018

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com