METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, January 26, 2018

DKT ANGELINE MABULA: ELIMU BURE HAIKUONDOLEI WAJIBU WAKO KAMA MZAZI

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wazazi kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora kwenye mazingira rafiki

Hayo ameyasema kata ya Nyamanoro akiendelea na ziara yake kwa halmashauri kuu za kata za chama cha mapinduzi kutoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi tangu Serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani ambapo amewataka wazazi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kumhudumia mwanafunzi na kushiriki katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na ubora wa elimu yenyewe itakayotolewa

'... Ndugu zangu naomba tunapotafsiri kauli za Mheshimiwa Rais tusitafsiri vibaya, Lile la elimu bure halikuondolei wajibu wako kama mzazi katika kumsaidia mwanao lile jukumu lako lipo pale pale ..' Alisema

Aidha Mhe Mbunge amewataka watumishi wa Umma kuwa waadirifu kwa kuunga mkono Sera na maelekezo ya Serikali na si kukwamisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo huku akiwaasa wanachama wa chama cha mapinduzi kuhakikisha wanaisimamia vizuri Serikali nakuacha kulalamika pembeni

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalumu wa kata hiyo Mhe Kuruthumu Abdallah amemuhakikishia ushirikiano mbunge huyo katika kutimiza utekelezaji wa Ilani na kisha kumpatia hati ya shukrani kwa niaba ya wananchi wa kata yake kama ishara ya kutambua jitihada kubwa anazozifanya katika kuwaletea maendeleo

Akihitimisha mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa kata ya Nyamanoro Mhe Patrick Mkwawa mbali na kumpongeza mbunge huyo kwa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ndani ya kata yake amesema kuwa anaridhishwa na kasi yake pamoja na kuwataka wanachama wengine kuendelea kumuombea na kumuunga mkono.

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
26.01.2018

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com