Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa tanga ndugu Omari Mwanga akiongozana na katibu wake tarehe 27/01/2018 wamefanya ziara wilayani Tanga mjini. Katika ziara hiyo mwenyekiti huyo alikutana na kufanya kikao na viongozi mbali mbali wa wilaya, kata na matawi.
Mwenyekiti huyo wa vijana alianza kwa kuwashukuru viongozi hao ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa vijana mkoa wa tanga kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kama mwenyekiti wao kwa kipindi cha mwaka 2017-2022. Aidha mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kuvunja rasmi makundi yaliyopo kabla na baada ya uchaguzi.
"Nachukua fursa hii kuvunja makundi yote yaliyopo kabla na baada ya uchaguzi sisi sote ni vijana na tunaunganishwa na itikadi ya chama cha mapinduzi tunapaswa kuungana kujenga jumuiya yetu imara " alisema ndugu Omari mwanga
Mwenyekiti huyo wa vijana mkoa aliwaagiza viongozi wa wilaya, kata na matawi kuunda vikundi mbali mbali vya vijana ili wapatiwe 5% za mapato ya halmashauri kama ilivyoelekeza serikali.
Pia aliwaagiza viongozi wa wilaya na kata kufanya ziara katika maeneo yao ili kutambua changamoto zinazowakabili vijana na kuzipatia ufumbuzi.
Mwisho, mwenyekiti huyo alimalizia kwa kuwaasa vijana wa wilaya ya tanga mjini kudumisha umoja, amani na upendo kati yao.
0 comments:
Post a Comment