METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, January 28, 2018

LUKUVI : LENGO LA SERIKALI NI KUPANGA, KUPIMA NA KUMILIKISHA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwenye makazi yenye thamani yaliyopangwa, kupimwa na kumilikishwa

Hayo ameyasema wilayani Ilemela kata ya Nyasaka wakati wa kukabidhi hati zaidi ya elfu Tano kwa wananchi wa wilaya hiyo kati ya wananchi elfu Kumi na Tano walionufaika na zoezi la urasimishaji wa makazi linaloendelea nchini nakutarajiwa kufika tamati mapema mwishoni mwa mwaka huu wa fedha ambapo amewataka wananchi Elfu Kumi waliosalia kuhakikisha wanalipia gharama za hati ili waweze kumilikishwa maeneo hayo ili kuyaongezea thamani huku akiisifu wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kuwa halmashauri pekee nchini iliyofanya vizuri zoezi hilo la urasimishaji wa makazi

'... Hakuna sehemu yeyote hapa nchini iliyofanya zoezi la urasimishaji vizuri kama Ilemela na Nyamagana mkoa wa Mwanza,  Kwahiyo nimekuja hapa kuwapongeza  watendaji na Viongozi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela mkuu wa mkoa amesimamia vizuri, watendaji wamesimamia vizuri na Naibu wangu Waziri amesimamia vizuri ...' Alisema

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amemshukuru Waziri huyo na Mhe Rais Dkt John Magufuli kwa zoezi hilo huku akimhakikishia kuendelea kumsadia kusisitiza juu ya umuhimu wa zoezi hilo kwa wananchi wake

Ikumbukwe kuwa Mhe William Lukuvi alikuwa na ziara ya siku mbili kwa wilaya ya Ilemela ilioanza kwa kutembelea maeneo yenye migogoro mikubwa ya Ardhi ikiwemo ule wa  wananchi na jeshi la wananchi, wananchi na uwanja wa ndege, wananchi na jeshi la polisi kisha kukagua mfumo wa Ardhi wa manispaa ya Ilemela na baadae kusikiliza kero za Ardhi za wananchi   kabla ya kuhitimisha kwa zoezi hilo la kukabidhi hati

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
28.01.2018

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com