METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, January 28, 2018

TUITUMIENI VIZURI MITANDAO YA KIJAMII

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amewaasa wananchi kuitumia vizuri mitandao ya kijamii katika shughuli za  maendeleo

Hayo ameyasema kata ya Kiseke Jimbo la Ilemela wakati wa muendelezo wa ziara yake ya utekelezaji wa Ilani ambapo amewaasa wananchi hao kuitumia vizuri mitandao hiyo ya kijamii kama chachu ya kuibua kero na changamoto zinazoikabili jamii yao na kisha kushirikiana na viongozi wa serikali katika kuzipatia ufumbuzi na si kuwa sehemu ya kuchochea mmomonyoko wa maadili na maovu katika jamii

'... Hii mitandao ya kijamii tukiitumia kwa kuchochea shughuli za maendeleo itatusaidia sana, Lakini tukiitumia vibaya itatuletea shida hivyo niwapongeze sana Viongozi wa Kiseke kwa kuwa wabunifu mmeunda lile kundi la whatsap na mmetunganisha Viongozi wote wakuu wa serikali na wananchi na tunaona namna mnavyotumia kundi lile katika kumaliza changamoto na kero za wananchi wenzetu ...' Alisema

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula hakuacha kusisitiza juu ya umuhimu wa zoezi la urasimishaji makazi linaloendelea nchini na wajibu wa mzazi katika kusaidia watoto wao kupata elimu bora ili kwenda sambamba na lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli kupitia Sera ya ELIMU BURE ili kusaidia wananchi wanyonge na masikini waweze kupata elimu na kujiletea maendeleo

Kwa upande wake Diwani  wa kata ya Kiseke Mhe Innocent Mwinyikondo amemshukuru Mbunge huyo kwa kuitembelea kata yake huku akieleza miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika kata yake kwa msaada wa mbunge huyo ikiwemo barabara kubwa ya lami ya kutoka Sabasaba kupitia Kiseke kwenda Buswelu, Ujenzi wa Kituo cha polisi,  ujenzi wa ofisi ya walimu, mradi wa maji, msaada wa tofali na uendeshaji wa zoezi la utoaji wa elimu ya ujasiriamali kupitia taasisi ya The Integrity foundation

Pamoja na hayo Mhe Angeline Mabula alitumia fursa hiyo kuwalipia gharama za matibabu kwa kadi  ( TIKA ) jumla ya wazee Kumi waliohudhuria mkutano huo na kisha kuendelea na ziara yake kwa kata ya Kitangiri

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
28.01.2018

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com