METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, January 28, 2018

KATIBU MKUU MIFUGO DKT MARIA MASHINGO AHAMASISHA UPIGAJI CHAPA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA

Zikiwa zimebaki siku nne (4) tu muda wa zoezi la upigaji chapa  kukamilika  January 31 mwaka huu kwa mujibu wa muda uliongezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina,Katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo atua Tabora Igunga  kuhamasisha upigaji chapa Dakika za mwisho.

Akiongeoa na wafugaji katika kijiji cha Simbo alipofika kushuhudia zoezi la chapa likiendela, Dkt.Mashingo amewaagiza wafugaji hao kuwambia wenzao waliopo huko porini ambao bado hawajapiga chapa mifugo yao wajitokeze kupiga chapa Mifugo yao kwani baada ya muda huo wa nyongeza kuisha hakutakuwa na nyongeza ya muda Mwingine.

"Hili Zoezi lilianza mwaka 2016 mpaka mwaka jana 2017 halikuweza kukamilika,Zoezi hili ni la kisheria,hata Mheshimiwa Rais analitambua,tunafanya hivi Ili kuzuia Wizi wa Mifugo,Kuzuia Mifugo kutembea ovyo,Kuzuia Magonjwa ya Mifugo yasiambukizwe kutoka sehemu nyingine na kwenda upande mwingine"alisema

Aidha Katibu Mkuu Mifugo amepokea taarifa ya Upigaji chapa mkoa wa Tabora iliyosomwa kwake na Kaimu Katibu tawala wa Mkoa huo Bw.Natalis Linuma kuwa Tabora inafanya vizuri katika utekelezaji wa zoezi hilo katika  Wilaya zake zote.

Linuma amezitaja Wilaya hizo kuwa ni Kaliua Dc imefikisha Asilimia 100.54,ya usajiri mifugo,Nzega Dc asilimia 95,Tabora Manispaa asilimia 92.02.

Zingine ni halmashauri ya Wilaya ya Urambo asilimia 101,Nzega Dc asilimia 84.12,Sikonge asilimia 83.20,Uyui asilimia 81.22 na Igunga asilimia 82.1

Vilevile Halmashauri ya Wilaya Igunga mbali na kutokufikisha asilimia Mia moja ya Upigaji chapa mifugo,lakini wamejiwekea Mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo kabla ya tarehe ya mwisho, Mikakati hiyo ni pamoja na kuwapa mafunzo ya Upigaji chapa Vijana watatu ambao halmashauri inawalipa vijana hao kila siku Tsh Elfu kumi.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida inasemekana baada ya wafugaji kuhamasika upigaji chapa Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kata simbo kijiji cha simbo,Mtendaji wa kijiji hicho huchukuliwa na baadhi ya Wafugaji usiku wa Manane  na kwenda kuwapigia chapa Mifugo yao kwa hofu kuwa isije ikafika tarehe 31 mwezi huu wakiwa bado hawajakamilisha.

Awali Katibu Mkuu Mifugo kabla ya kukaribishwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri katika oparesheni ya Upandaji Miti ya Vyama vya siasa,alipata fursa ya kuuangalia mti aliupanda mwezi mmoja uliopita katika eneo la Ipuli Manispaa ya Tabora.

Dkt. Mashingo ameongea na vyombo vya habari juu ya Umuhimu wa zoezi hili la upigaji cha Mifugo nchi nzima na kuwataka wafugaji kuchangamkia kusajiri Mifugo yao kwani baada ya zoezi hilo kukamilika serikali itatoka msimamo wake kwa Mifugo yote ambayo haijapigwa picha.

Pia katibu Mkuu Mifugo amepata fursa ya kutembelea mnada wa Upili wa Ipuli uliopo Manispaa ya Tabora na Mnada wa Igunga Uliopo halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com