Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na mmoja wa mafundi kwenye ukikagua wa ujenzi wa daraja la Twangoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Twangoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Twangoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na msimamizi wa ujenzi wa daraja la Twangoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Twangoma
Eneo la ujenzi wa daraja ukiendelea
.........................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe. Selemani Jafo, leo amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika daraja la Twangoma ili kujionea uhalisia wa ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiungo muhimu kwa wakazi wa Mbagala na maeneo ya Twangoma jijini Dar as salaam.
Waziri Jafo amefanya ziara hiyo kwa lengo la kupata ukweli wa utendaji kazi katika ujenzi wa daraja hilo ambao unafanywa chini ya Ofisi yake ya TAMISEMI kupitia mradi wa DMDP.
Katika ziara yake, Jafo amefika eneo la mradi asubuhi na mapema na kuwakuta Vijana wakiwa kazini huku ujenzi huo ukienda kwa kasi kubwa.
Waziri Jafo amewataka wakandarasi wengine kuiga mfano huo wa uchapaji kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
0 comments:
Post a Comment