METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 31, 2018

DC BUSEGA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI MWAKA 2018

Imehaririwa na Mathias Canal, WazoHuru Blog

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Mhe Tano Mwera amezindua rasmi kampeni ya upandaji miti kwa mwaka  2018 itakayohamasisha wananchi kupamba miti ili kukabiliana na kadhia mbalimbali zinazokutikana kutokana na miti kukatwa ovyo.

Dhifa ya uzinduzi huo imefanyika katika shule ya Secondari Anthony Mtaka ambapo uongozi wa Wilaya ya Busega umeshirikiana na shirika lisilo la kiserikali la "TUJENGE " linalofadhiliwa na "Umoja wa Ulaya, lenye kauli mbiu ya " Tuungane Kutetea Haki" jana tarehe 30 Januari 2018.

Hilo ni zoezi la kitaifa ambapo kila Wilaya inatakiwa kupanda miti takribani milioni moja na nusu kila mwaka ili kufanikisha zoezi hilo la Halimashauri ya wilaya hiyo.

Katika shughuli ya upandaji miti Halamshauti ya Wilaya ya Busega  imegawa miche ya miti kwa taasisi mbalimbali za serikali zikiwemo shule, zahanati na vituo vya afya sambamba na wananchi wa kawaida.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa wilaya ya Busega Mhe Tano Mwera  imeitaka kila kaya kupanda miti 48 ya matunda na kivuli.

Mhe Mwera ametoa onyo Kali kwa wananchi wanaokata miti ovyo kwa ajili ya nishati ya mkaa bila kufuata utaratibu kuacha Mara moja kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na serikali itamchukulia hatua Kali za kisheria kila atakayekiuka agizo hilo.

Pia amewataka waliopewa miti kuhakikisha wanaiotesha na kuilinda mpaka ikue.

Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Wilaya hiyo amemtaka Mkurugenzi wa Halimashauri ya Busega Ndg Anderson Njiginya kuhakikisha anasimamia kikamilifu zoezi la upandaji wa miti na kuandaa mpango kazi wa kuwezesha kila shule kuwa na bustani za miche ya miti/ Vitalu ili kusaidia upatikanaji wa miche ya miti ya matunda na vivuli.

Pia amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kusimamia zoezi la upandaji miti pembezoni mwa barabara ya Lamadi kwenda Bariadi.

Akizungumza katika uzinduzi huo mratibu wa "TUJENGE", Ndg Josephat Kaigwa amewaasa wanafunzi kukua katika maadili mema ya kutunza mazingira sambamba na kupiga vita rushwa.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com