Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturuwakati wa kikao cha kazi
Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo (Aliyesimama) akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Mwingine ni Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu (Katikati), Afisa Kilimo na Mifugo
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo (Kulia), Mwingine ni Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor
Na
Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu amekutana na kufanya kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Mifugo,
Ardhi, Maliasili na mazingira kubaini kwa pamoja mbinu bora za kuwasaidia
wakulima kuzalisha mazao ya chakula na biashara kwa wingi.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa
na Maafisa kilimo na Mifugo, Maafisa Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maafisa
Ugavi wa Kata sambamba na Maafisa Tarafa, Mhe Mtaturu alisema kuwa bado
uzalishaji wa mazao ni mdogo katika Wilaya ya Ikungi ukilinganisha na hali ya
hewa ikiwa ni pamoja na kuwa na ardhi nzuri.
Aliwataka wataalamu hao wa kilimo kuwasaidia
wakulima ili kuiwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kuwa kilimo
cha kibiashara kitakachowezesha kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupunguza
umasikini kwa watanzania Sambamba na kujitosheleza kwa chakula.
Mhe Mtaturu alisema Ili kuwe na
kilimo kizuri na tija kwa wananchi, Wataalamu mnapaswa kuzingatia uwepo wa
Pembejeo za kilimo na mbegu Bora za kisasa ambazo zinazalisha mazao mengi
sambamba na kuhuisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuandaa mpango wa kujenga skimu
za umwagiliaji ili wananchi waweze kuzalisha chakula cha kutosha mwaka mzima.
Alisema kuwa ili kuongeza uzalishaji
wa mazao ya kilimo tayari serikali imetoa tani 20 za mbegu za Pamba katika
Wilaya ya Ikungi ambazo zitagawanywa kwa wakulima ili msimu wa kilimo
unapoanza tayari ukata wa kucheleweshwa kwa mbegu hizo uwe umetekelezwa.
Pia aliwaagiza maafisa ugani kuwa na
mashamba darasa kwani kupitia wao yatawasaidia wakulima kuwa na uelewa mkubwa
katika kuongeza ufanisi wa kilimo chenye tija.
Aidha, Alisema kuwa Katika
kutekeleza majukumu ya wananchi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
imeanzisha huduma zake kanda ya Kati Dodoma kwa kulenga mnyororo wa ongezeko la
thamani katika mazao ya kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa
kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini
Tanzania.
Mhe Mtaturu alisema ni vyema kama Wataalamu wa
Kilimo watatumia nafasi hiyo kuwaunganisha wakulima na Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB) kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza
Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo.
Katika kikao hicho Cha kuwakumbusha
majukumu wataalamu hao Mhe Mtaturu amewataka kuandaa mpango kazi wa mazao ya
Kilimo hususani mazao ya chakula na Biashara.
Mhe Mtaturu aliwaelekeza wataalamu
hao wa kilimo kuwasisitiza wananchi katika maeneo yao kuanza kulima mazao ya
kipaombele yaliyoelekezwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ambayo Ni zao la
Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.
Alisema pomoja na mazao hayo ya
kipaumbele lakini pia wananchi wanapaswa kuendelea kuongeza nguvu katika mazao
yanayostawi kwa wingi Wilayani humo ikiwa Ni pamoja na zao la Alizeti, Mtama,
Mahindi na zao la Dengu.
Katika upande mwingine Mhe Mtaturu
alishauri wataalamu wa Mifugo kutilia msisitizo Ufugaji wa kisasa (Ziro
Grazing) kwa kutembelea na kupata utaalamu wa Ufugaji na mbegu Bora za ya
Ng'ombe wa kisasa kwa wataalamu katika Rachi ya Taifa ya Kongwa (NARCO) na LITI
iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa
Wilaya aliagiza heka 1500 ambazo ni kichaka kuandaliwa utaratibu kwa ajili ya
kilimo ili kuongeza uzalishaji wa kilimo.
Naye Afisa Kilimo na Mifugo
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo alipongeza kasi ya uwajibikaji
ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa ufanisis wake katika
uwajibikaji na kusaidia kuonyesha njia jambo ambalo linapelekea kubadili fikra
za wakulima na wananchi kwa ujumla.
Sengo Alimpongeza Mkuu huyo wa
Wilaya ya Ikungi kwa kuwezesha kupatikana muwekezaji ambaye atapewa heka 1000 Na
serikali ya kijiji kwa ajili ya kilimo cha korosho zao ambalo litakuwa na tija
kwa pande zote mbili kwani pia wananchi watanufaika na huduma za ugani na
kuweka mkakati wa namna kijiji kitakavyonufaika na uwekezaji huo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment