Muwezeshaji
wa Mafunzo kuhusu Mpango wa Matumizi bora ya ardhi kutoka Shirika la PELUM
Tanzania, Josent Tesha akifafanua jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Ugesa Wilaya
ya Mufindi Mkoani Iringa kuhusu manufaa na faida ya mpango huo hivi karibuni.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la Pelum na kufadhiliwa na Shirika la
Misaada la Marekani (USAID).
Mwezeshaji
wa Mafunzo kuhusu Mpango wa Matumizi bora ya ardhi kutoka Shirika la PELUM
Tanzania, Simon Mbago akifafanua jambo
kwa wananchi wa Kijiji cha Ugesa Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kuhusu manufaa
na faida ya mpango huo hivi karibuni. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la
Pelum na kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Na
Mwandishi Wetu, Morogoro
SHIRIKA
la PELUM Tanzania kupitia Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika sekta ya kilimo
(CEGO) limefanikiwa kutoa elimu ya mafunzo kuhusu Mpango wa Matumizi bora ya
ardhi kwa wananchi4,270 kutoka Mikoa ya
Morogoro, Dodoma na Iringa.
Akizungumza katika
mahojiano maalum na Mwandishi wa Habari hii Mjini Morogoro, Afisa Tathimni na
Ufuatiliaji wa Shirika la PELUM Tanzania Frank Maimu alisema katika awamu ya
kwanza shirika hilo lilitoa mafunzo kwa wananchi 3,070 na awamu ya pili
wananchi 1200 na na tathmini yao ilibaini kuwa kuna uhitaji mkubwa wa wananchi
wengine kupatiwa elimu hiyo.
Maimu alisema kuwa,
kupitia mradi wa CEGO unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani
(USAID), Shirika hilo lilihakikisha kuwa wananchi wanapatiwa elimu ya masuala ya
ardhi kama njia mojawapo ya kuhakikisha mpango huo unakamilika kwa ridhaa ya
wananchi wenyewe.
“Katika mafunzo hayo tunatoa elimu kupitia mada mbalimbali ikiwemo Mpango wa matumizi ya ardhi
kijijini, haki za ardhi kwa wanawake, haki ya kupata, kutumia na kumilikia ardhi
Tanzania, utatuzi wa migogoro ya ardhi Tanzania pamoja na utawala wa
kidemokrasia katika Jamii” alisema Maimu.
Aliongeza kuwa kupitia
mafunzo hayo ya mipango ya matumizi ya ardhi vijijini, wananchi hao pia
waliweza kuelimishwa njia mbalimbali za kutatua migogoro ya ardhi,
kufahamu umuhimu na haki wa kumiliki ardhi kwa makundi
mbalimbali pamoja na wananchi kuweza kusimamia Serikali zao kuanzia ngazi za
vijiji.
Kwa mujibu wa Maimu
alisema mbali na wananchi wa kawaida makundi mengine yaliyopatiwa mafunzo hayo
kuwa ni pamoja na kamati za maamuzi, mabaraza ya ardhi ya kijiji, mabaraza la
kata pamoja na Halmshauri za vijiji.
Kwa upande wake Devota
Winga kutoka kijiji cha Nchinila Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma anasema kupitia
mafunzo yanayotolewa na Shirika la PELUM Tanzania ameweza kufahamu haki zake za
msingi katika masuala ya ardhi ikiwemo
sheria ya umiliki wa ardhi jambo ambalo halikuwepo katika jamii zao siku
za nyuma
Naye Kaimu Afisa Mtendaji
wa kijiji cha Iduo Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Bi. Ashura Elianaki anasema idadi ya kesi za migogoro ya ardhi
iliyokuwa ikiripotiwa katika Serikali ya Kijiji hicho kwa sasa imepunguakwani
kwa sasa wananchi wengi wameweza kuelimika kupitia mafunzo ya Shirika la PELUM
Tanzania.
“Wananchi wengi sasa
wameweza kuelewa na kufahamu kwa undani wa sheria zinasemaje na na aina ya kesi
zinazopaswa kutafutiwa suluhu na zipi zinapaswa kusuluhishwa na vyombo vingine kwa
kuanza kusikilizwa na Baraza la Ardhi la Kijiji na sio Serikali ya kijiji”.alisema
Elianaki.
Mbali na PELUM Tanzania
kutoa mafunzo kwa wananchi wananchi 4,270 na kutekeleza Mpango wa matumiz ya
Ardhi kwa vijiji vya mradi, Shirika hilo pia linatarajia kutoa hatimiliki za
kimila 4883 kwa vijiji 25 vya awali ambavyo vimeshafanyiwa Mpango wa matumizi
ya Ardhi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment