Watumishi wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiingiza taarifa za wananchi kwenye
mfumo wakati wa zoezi la usajili linaloendelea katika ofisi ya kata ya
Lubaga, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Hawa ni baadhi tu ya wananchi
ambao kamera yetu imewanasa wakisubiri huduma ya Usajili katika zoezi
linaloendelea la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa lengo la kuwapatia
Vitambulisho vya Taifa.
Kina mama na wazee waliojitokez
kusajili katika Kata ya Lubaga wakisubiri kuitwa majina kuingia chumba
cha Usajili kupata huduma.
……….
Wananchi mkoani Shinyanga
wamesema wamefarijika kuona kuanza kwa zoezi la Usajili Vitambulisho vya
Taifa kwani ni zoezi ambalo wamekuwa wakilisikia kwa muda mrefu na
hatimaye nao wamefikiwa na kupata fursa ya kujisajili.
Akizungumza wakati zoezi hilo
likiendelea mmoja wa kutoka kata ya Lubaga Shinyanga Mjini amesema “kwa
muda mrefu tulikuwa tukisubiri kuanza kwa zoezi hili kwani wananchi
tunapata shida hususani wakati tukiwa tunataka kupata huduma mbalimbali
ambazo zinalazimu mtu kuwa na Kitambulisho cha Taifa, hivyo hii ni fursa
kwa wakazi wote wa Shinyanga kuweza kujitokeza Kusajiliwa”.
Baadhi ya huduma ambazo sasa
zimeanza kutolewa wa kutumia Vitambulisho vya Taifa ni huduma ya
kusajili namba za simu, Huduma za Benki, kutambulika kwenye huduma kwa
Kaya masikini kirahisi na huduma nyinginezo.
Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa
mikoa katika Kanda ya Ziwa ambapo zoezi hilo linaendelea kwa sasa
likihusisha uchukuaji alama za kibaiolojia, picha na saini ya
Kilelektroniki. Mikoa mingine ni Mara, Mwanza, Simuyu, Geita, Singida,
Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Songwe.
0 comments:
Post a Comment