Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi wa Mkoa wa Iringa
mara baada ya kusomewa taarifa ya maendeleo ya sekta ya kilimo Mkoani humo na
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza, Jana Disemba 4, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa akisalimiana na Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza
Achali ya nyanya/TOMATO SOURCE cha Chai Bora Ltd/Dabaga Ndg Sanjay Rai
kilichopo Kijiji cha Ikokoto Kata ya Ilula Wilayani Kilolo Mkoa wa Iringa alipotembelea kiwanda hicho sambamba na kufanya mkutano na
wawakilishi wa wakulima. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe Asia Abdalah
Juma, Jana Disemba 4, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa akisalimiana na Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza
Achali ya nyanya/TOMATO SOURCE cha Chai Bora Ltd/Dabaga Ndg Sanjay Rai
kilichopo Kijiji cha Ikokoto Kata ya Ilula Wilayani Kilolo Mkoa wa Iringa alipotembelea kiwanda hicho sambamba na kufanya mkutano na
wawakilishi wa wakulima. Jana Disemba 4, 2017.
Mkuu Wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza akisoma taarifa ya hali ya sekta ya chakula katika mkoa huo mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa . Jana Disemba 4, 2017.
Picha ya pamoja Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa (Wa tatu kulia) Mkuu Wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza (Wa pili
kulia) Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi Wamoja Ayubu, Mkuu wa Wilaya ya
Mufindi Mhe David Willium Jamhuri na wataalamu wa Kilimo Mkoa wa Iringa. Jana
Disemba 4, 2017.
Na Mathias Canal, Iringa
Wakulima wa zao la Nyanya wametakiwa
kuondoa wasiwasi wa kufikiri kupunguza kasi ya kilimo kutokana na viwanda vya
nyanya kununua tani chache za nyanya tofauti na uzalishaji.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikokoto
kilichopo Kata ya Ilula Wilayani Kilolo Mkoa wa Iringa mara baada ya kutembelea
kiwanda cha kutengeneza Achali ya nyanya/TOMATO SOURCE cha Chai Bora Ltd/Dabaga.
Alisema kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho
kipya ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda hivyo
kitawanufaisha wakulima hao wa nyanya ambao soko lao linasuasua.
Alisema kuwa kiwanda hicho ambacho
kilianza uzalishaji Octoba mwaka huu kwa kuchakata nyanya kwa Tani 16 mpaka
Tani 20 kwa masaa 8 pindi kitakapokamilika na kuanza kufanya kazi kwa masaa 24
kitaongeza uzalishaji hivyo wakulima wa nyanya watapata soko la uhakika.
Mhe Mwanjelwa aliwahakikishia wakulima hao
kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wakulima nchini ili waweze
kunufaika na kilimo kwani inafahamika kuwa asilimia zaidi ya 75 ya watanzania
wanajihusisha na kilimo.
Aliwasihi wakulima hao Kulima nyanya kwa
awamu tofauti na hivi sasa ambapo wanalima kwa msimu kwani kufanya hivyo
itawasaidia kupata kipato wakati wote huku viwanda vikiwasaidia kununua mazao
hayo wakati wote kwani kwa sasa viwanda hivyo vinafungwa kutokana na msimu wa
nyanya kumalizika.
Aidha amewasihi wamiliki wa kiwanda cha
kutengeneza Achali ya nyanya/TOMATO SOURCE cha Chai Bora Ltd/Dabaga kuwa na bei
rafiki kwa wakulima kwani kufanya hivyo itakuwa ni msingi wa kuinua kipato cha
mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.
Sambamba na hayo pia alisisitiza Uongozi
wa Vijiji na Kata kusaidiana na wataalamu wa ushirika na maendeleo ya jamii
kuendelea kuhamasisha wakulima kujiunga katika vikundi vya Vyama vya ushirika
ili waweze kupata mikopo ya fedha, pembejeo na kupata mafunzo ya ugani na
kuanzisha viwanda vidogo vya kusindika mazao wanayozalisha.
Wakati huo huo Naibu Waziri huyo wa kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa amesifu juhudi za uongozi wa Mkoa wa Iringa unaoongozwa na
Mkuu wa Mkoa huo Mhe Amina Masenza kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwa ni pamoja
na kuanzisha kampeni ijulikanayo kama “Mkoa Wetu, Viwanda Vyetu” yenye
lengo la kuwezesha wakulima kupata masoko ya uhakika kwa mazao wanayozalisha.
Aidha, ameelekeza kuchukuliwa hatua kali
za kisheria kwa wafanyabiashara wote watakaobainika kukiuka bei elekezi ya
mbolea katika Mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment