METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 4, 2017

BUSEGA YAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Na Mwandishi Wetu, Simiyu

Kila ifikapo tarehe 01 Desemba Ulimwengu Mzima huadhimisha siku ya UKIMWI Duniani ambapo katika Mataifa mbalimbali huungana na malengo ya milenia ya kufikia mwaka 2020 kupunguza maambukizi na kuifanya jamii ambayo imethiriwa kutumia dawa za kuongeza maisha na kutowanyanyapaa watu wenye maambukizi.

Kama ulivyo umuhimu wa kusihi pia Siku hii ni maalumu kwa ajili ya kuwakumbuka walipoteza maisha kwa kutokana na UKIMWI ili kukumbushana na kupeana majukumu ya jinsi ya kukabiri kadhia hili.

Katika Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu  maadhimisho haya yamefanyika Kijijini  Nyamikoma, Kata ya Tabitha ikichagizwa na Kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Changia Mfuko Wa Udhamini Wa Ukimwi, Okoa Maisha".

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Busega ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mhe Tano Mwera alisisitiza wananchi kutambua kuwa Ugonjwa Wa Ikimwi ni hatari hivyo wanapaswa kujinga na maambukizi mapya.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Busega Dr Fredy Mruma alikaririwa akisema " Kwa ujumla maambukizi ya VVU/UKIMWI Wilayani Busega kwa sasa ni asilimia 4.5% na sehemu zenye maambukizi makubwa kwa sasa ni maeneo ya Mialo hasa Mwalo wa Ihale".

Alisema Ili kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI Halmashauri ya Wilaya ya Busega imeweza kuhamasisha matumizi ya Kondomu, Kugawa kondomu katika maeneo yenye hatari ya kupata maambukizi mengi ya VVU (High Transmission Area) kama kandokando ya barabara kuu, mialoni, na maeneo yaliyo karibu na magulio na minada ya ng'ombe.

Aliongeza kuwa Kuelimisha wajawazito juu ya kuzuia maambukizi ya VVU kwa mtoto kutoka kwa mama na pia utoaji wa dawa kwa wajawazito waliobainika kuwa na VVU ili watumie kwa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Kutoa mafunzo ya jinsia, stadi za maisha kwa vijana walio shuleni (Wanafunzi wa darasa la tano hadi kidato cha nne) na walio nje ya shule kwa nia ya kupunguza maambukizi ya VVU kwa njia ya kushiriki ngono zembe na Kuhamasisha jamii ili wapate huduma ya ushauri nasaha na kupimwa VVU.

Hata hivyo Huduma ambayo hutolewa katika vituo 6 vilivyoanzishwa Wilaya ya Busega, vituo vya afya vya Igalukilo, Badugu, Mkula, Nassa, Lukungu na Nyamikoma.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe Tano Mwera aliwaasa wananchi kuepukana na mienendo inayopelekea maambukizi ya UKIMWI kama vile ulevi wa kupindukia, jadi zinazohusisha kurithi wajane, ukeketaji wa wanawake, namna ya kutoa matibabu asili, ikiwa pamoja na uchanjaji kwa kutumia viwembe vinavyotumika na watu wengi na ngono zembe.

Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupima UKIMWI ili kama wana maambukizi waanze kutumia dawa mapema ili kurefusha maisha yao.

Alisema kuwa uoga hauna tija kwani uoga hautageuka kuwa tiba kama "UKIMWI unao, unao tu ni vizuri kukubali matokeo. Pia amewataka watendaji wa halmashauri  kufanya shughuli zao kwa kushirikisha viongozi wa ngazi zote na kada zote ili huduma hizi ziweze kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Pia aliwashauri wale ambao tayari wanatumia dawa wasiache katikati kwa kusikiliza maneno ya watu. Wasikilize ushauri wa  wataalumu tu na wafatilie dozi zao kwa ajiri ya afya zao.

MWISHO.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com