Richmond
Raymond akipokewa na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mwanza baada ya
kuwasili na tuzo za ushindi akitokea nchini Afrika ya Kusini
Msafara wa kutoka uwanja wa ndege kupokea cheti cha tuzo
Baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kupokea tuzo ambayo kiwanda kimetunukiwa
Baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kupokea tuzo ambayo kiwanda kimetunukiwa.
Baada ya
kutumikiwa tuzo kubwa ya Mackay Award ya SABMiller kutokana na kufanya
uzalishaji usiochafua mazingira hivi karibuni,wiki iliyopita kiwanda cha
TBL cha Mwanza kuchomoza katika mashindano ya viwanda vya bia na
kutangazwa kuwa ni kiwanda bora kinachoshikilia nafasi ya pili kwa ubora
barani Afrika baada ya kushindanishwa na viwanda vingine 21 kutoka nchi
mbalimbali.
Kiwanda
cha TBL Mwanza ni kiwanda pekee barani Afrika ambacho kinatumia
teknolojia ya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga hali ambayo
imepunguza kasi ya uharibifu wa mazingira utokanao na mchakato wa
uzalishaji viwandani.
Mbali na
kutumia teknolojia hii rafiki kwa mazingira kiwanda hiki pia kimekuwa
kinara kwa kuzalisha bidhaa bora na kimeleta chachu ya kukua kwa
shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Mwanza ikiwemo kuongeza fursa za
ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa wananchi bila
kusahau kuendesha kampeni za matumizi mazuri ya maji na utunzaji wa
mazingira.
Akiongelea
mafanikio ambayo kiwanda kimeyapata,Richmond Raymond, aliyekuwa Meneja
wa kiwanda hicho ambaye kwa sasa amehamishiwa kikazi nchini Afrika ya
Kusini alisema kuwa ushindi huu umetokana na Uwekezaji makini uliofanywa
na kampuni bila kusahau juhudi za pamoja za wafanyakazi wake.
0 comments:
Post a Comment