Chama cha Wanawake Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi
na Mazingira, Tanzania Association of Women Leaders in Agriculture and Environment ( TAWLAE) leo wamefungua
rasmi mkutano wa mwaka wa 21 ambao mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bi Butano
Philipo kwa niaba ya Waziri wa Mazingira
Mhe. January Makamba, mkutano ambao umefanyika leo katika Viwanja vya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Maadhimisho hayo ya 21
yamebeba kaulimbiu isemayo Uchumi wa Viwanda Tanzania Wanawake tupo tayari, hapa kazi tu.
Aidha Dkt. Sofia Malote amesema kazi ya TAWLAE ni
kuwaunganisha wakulima wadogo au wakubwa na tafiti mbalimbali ambazo zimetafitiwa hapa nchini ili kuongeza uwekezaji na ajira kwa
watanzania katika kilimo.
Akizungumza katika
wasilisho lake Dkt. Malote amesema kilimo kilikuwa na faida ndogo kwa sababu utalaamu, teknolojia
na juhudi zilikuwa bado hazijatumika vizuri kwenye kilimo hivyo ni jukumu la
TAWLAE kuhakikisha kuwa wanaleta mapinduzi ya kilimo katika uchumi wa viwanda.
Ili kuingia katika uchumi wa viwanda ni lazima uzalishaji wa kilimo uwe na tija, kuwepo na uboreshaji wa masoko na
teknolojia ambapo wataalamu wanawake ndio wanajukumu kubwa katika kuleta
mapinduzi ya kilimo alisema Dkt.Malote
Mwenyekiti wa chama cha wanawake viongozi TAUWLAE Dkt.
Sofia Malote wakati akiongea na wanachama katika mkutano wa 21 uliofanyika leo katika Viwanja vya Mifugo
0 comments:
Post a Comment