Jeshi
la Polisi Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maafisa wa Uhifadhi wa
Wanyamapori wamefanikiwa kumkamata jangili akiwa na meno ya Tembo 5
yenye thamani ya MIL 100 name mshitakiwa yuko kituo cha Polisi morogoro.
Sehemu ya shehena ya meno ya tembo iliyokamatwa. |
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei akiongelea tukio hilo, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliejulikana kwa jina la Nehemiah Nashon akiwa katika chumba namba 104 cha Hoteli ya BZ iliyopo maeneo ya Nane-nane Mjini Morogoro, na kwamba vipande hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi Mil. 100.
Jangili sugu akiwa na shehena ya meno ya tembo akiwa chini ya ulinzi mkali. |
0 comments:
Post a Comment