METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 5, 2017

MD KAYOMBO: PAMOJA NA KUTOA VITAMBULISHO KWA WAZEE TUNA MIKAKATI ZAIDI YA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam imempongeza waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu (Mb) kwa kuzindua zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya Tiba kwa wazee katika Manispaa ya Ubungo zoezi lililofanyika jana Septemba 4, 2017 katika uwanja wa TP Sinza E.

Katika ukurasa wake wa facebook Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ametoa pongezi hizo kwa waziri Ummy kwa kutoa Bima za afya kwa watoto 100 wenye umri chini ya miaka 18 pamoja na ahadi ya kujenga wodi ya wazazi, watoto na maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya katika Wilaya ya Ubungo

Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com umezungumza na Mkurugenzi Kayombo ili kujua kama kutolewa vitambulisho hivyo kwa wazee ndio mafanikio ya sekta ya afya ambaye alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili sekta ya afya ikiwa ni pamoja na gharama za uendeshaji wa huduma za Msamaha kwani zinmekuwa ni kubwa hususani katika Hospitali ya Sinza.

Zingine ni ufinyu wa nafasi ya wodi ya kulaza wagonjwa pamoja na kutokuwa na chumba cha kuhifadhi maiti (Mortuary), Upungufu wa watumishi wakiwemo madaktari, wauguzi na wataalamu wa maabara, sambamba na Upungufu wa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulace).

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa pamoja na changamoto hizo katika sekta ya Afya zinazoikabili Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo lakini kuna mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kutenga fedha zaidi ya 33.3 %  kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba katika mwaka wa fedha 2017/2018.

Kutengwa fedha kiasi cha Tsh 200,000,000/= katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa ghorofa 4 katika hospitali ya Sinza.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com