METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 26, 2021

JAMII YATAKIWA KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stansalus Nyongo akizungumza katika kikao kilichowakutanisha Kamati hiyo na Wizara ya Afya-Idara ya Maendeleo ya Jamii kuwapitisha katika mikakati ya Serikali ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kilichofanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika kikao kilichowakutanisha na Wizara kupitisha katika mikakati ya Serikali ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kilichofanyika jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Neema Lungangira akitoa mchango wake wa nini kifanyike katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kikao kilichokutanisha Kamati hiyo na Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.

Mtaalam wa masuala ya jinsia Dkt. Katanta Simwanza akielezea changamoto mbalimbali zinazotokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika kikao kilichowakutanisha na Wizara kupitisha katika mikakati ya Serikali ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya-Idara ya Maendeleo ya Jamii Sayi Magessa akielezea lengo la kikao kilichowakutanisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Wizara akieleza utekelezaji wa mikakati ya Serikali ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kilichofanyika jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeitaka jamii ya kitanzania kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.

Hayo yamebainika leo jijini Dodoma katika kikao kilichokutanisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii na Shirika la UNFPA kilicholenga kujadili jinsi ya kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokea katika jamii na hivyo Jamii inawajibu wa kukomesha vitendo hivyo.

Ameongeza kuwa elimu inahitajika kwa kiasi kikubwa kwa jamii katika kuhakikisha inabadili mitazamo ambayo kwa kiasi kikubwa inasababisha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika familia na jamii

“Tukifanikiwa kubadili mitazamo ya jamii zetu katika baadhi ya mambo hasi itasaidia sana kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii zetu” alisema Mhe. Nyongo

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali likiwemo shirika la UNFPA katika kuhakikisha inawafikia jamii hasa za vijijini katika kuwapatia elimu katika midahalo na mikusanyiko mbalimbali kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili kwa ustawi wa jamii

Naibu Waziri Dkt. Mollel ameongeza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii zetu vinatokana malezi na makuzi ndani ya Jamii.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com