Selasini
ametoa ombi hilo bungeni mjini Dodoma jana Alhamisi Novemba 9,2017
jioni akichangia mjadala wa mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa Taifa
kwa mwaka 2018/19 na mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti kwa
mwaka 2018/19.
Mbunge
huyo wa Rombo akichangia alisema mbunge huyo alishahusishwa na mauaji
ya mpenzi wa mpenzi wake, hivyo ni vyema akahusika na uchunguzi huo.
Baada
ya mbunge huyo kueleza hayo, Mlinga aliomba kwa Spika ampe taarifa
Selasini akisema katika kipindi cha uhai wake hajawahi kuhusishwa na
mauaji.
“Ninamheshimu
sana mheshimiwa Selasini. Tangu nizaliwe sijawahi kuhusishwa na kifo
cha mpenzi wa rafiki yangu namuomba alete ushahidi katika Bunge hili ni
nani alinihusisha,” alisema Mlinga.
Mwenyekiti
wa Bunge, Nagma Giga alimuuliza Selasini kama anapokea taarifa hiyo
lakini mbunge huyo aliendelea kushikilia msimamo wake akisema suala hilo
liliandikwa katika gazeti la Dira.
“Nimemsikia
na huo ni mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu ni mchungu. Gazeti la
Dira liliandika vizuri sana kuwa mpenzi wako alikusaliti. Wewe na kundi
la vijana wenzako mkaenda kumuua. Liliripotiwa polisi na limeripotiwa
kwenye magazeti na hujawahi kukanusha hadi leo,” alisema.
Selasini
alisema, “Ningeiomba Serikali katika uchunguzi wa nani waliohusika
kutaka kudhulumu maisha ya Tundu Lissu, huyu ambaye ameshatajwa kwamba
alihusishwa na mauaji uchunguzi uanzie kwake,” alisema.
Mbunge
huyo wa Rombo alisema asubuhi wakati Mlinga alipoomba mwongozo wa
Spika, mwongozo wake ulijaa kejeli na kumhusisha Kiongozi wa Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na mauaji ya albino.
Katika
mwongozo huo, Mlinga alihoji hatua ya Mbowe kutaka wachunguzi wa
kimataifa kuchunguza tukio la Lissu aliyejeruhiwa kwa risasi Septemba 7
mjini Dodoma na kuhoji ni kwa nini hakuwahi kutaka wachunguzi hao katika
mauaji ya albino.
Mlinga
alisema kwa kuwa kuna taarifa kuwa wapo wanasiasa wanahusika na mauaji
ya albino basi Mbowe naye ni mhusika na pia akasema ni kwa nini hakuhoji
mauaji ya watu wa Kibiti na Rufiji.
Hata
hivyo, Spika Job Ndugai alisema kwake haoni kama kuna mwongozo na
kuelekeza shughuli za Bunge ziendelee kwa wachangiaji kuanza kuchangia
mpango huo.
Asubuhi
katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Mbowe
alimuomba waziri mkuu akubali wachunguzi wa kimataifa waje nchini
kuchunguza tukio la kushambuliwa Lissu ambaye anaendelea na matibabu
katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Akijibu
swali hilo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema bado vyombo vya
kiuchunguzi nchini havijashindwa kuchunguza tukio hilo na
akawahakikishia Watanzania kuwa uchunguzi unaendelea.
0 comments:
Post a Comment